Searching...
Image and video hosting by TinyPic
13 August 2014
Wednesday, August 13, 2014

CR7 hakamatiki.


Na Oscar Oscar Jr

Hiki ndicho unachoweza kusema pale unapoamua kuacha kulala na kumtazama Mr Ballon D'or, Christiano Ronaldo. Akiungana na wachezaji wapya wa Real Madrid, Toni Kroos na James Rodriguez, pamoja na shujaa wa nyumbani, Gareth Bale, alifanikiwa kuipatia klabu yake ya Real Madrid mabao yote mawili na kunyakua kombe la UEFA Super kwa ushindi wa 2-0 dhidi ya Sevilla Jumanne.

Kiungo Kroos na Rodriguez walitamba sana kwenye fainali za kombe la dunia na kumfanya bosi wa Real Madrid Florentino Perez kufungua pochi yake na kumwaga pesa na kisha kuwaleta majushaa hao ndani ya dimba la Bernabeu.

Nahodha huyo wa Ureno alifungua udhia baada ya nusu saa kukatika pale alipofunga kutokana na krosi ya Bale na muda mfupi baada ya mapumziko, alifyatua kombora ambalo goli kipa wa Sevilla Beto hukuweza kuwa na namna yoyote ya kuzuia mpira licha ya kuufikia kwa mkono wake. 

Mpaka mwisho wa mchezo, Real Madrid 2-0 Sevila.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!