Barua ndefu kwa TFF: Sehemu ya tatu na ya mwisho.
Na Abuu Hozza
0759422148
Tumechagua kukumbatia majungu na kuukataa ukweli. Kubadili makocha wazungu kila siku haiwezi kuwa suluhisho, na hii inanifanya niamini msemo wa kuwa,”ni ngumu kwa tabia za kale kufa haraka”. Wapo wanolalamika kuwa tuna tatizo la uwepo wa wachezaji wengi wa kigeni katika ligi yetu.
Hii inazidi kutudanganya, hivi kwa Ramadhani Singano kucheza na Hamisi Tambwe hakumfanyi azidi kuwa bora? Domayo kucheza na Niyonzima hakumfanyi ajifunze mengi? Mbona hatulalamikii wingi wa makocha wa kigeni vilabu vyetu, au timu yetu ya taifa kuwa na utaratibu wa kufundishwa na makocha wa kigeni kila mara?
Kuna wachezaji wengi sana wa kibongo katika ligi yetu wala hilo sio la kulalamika, sema tunachokosa ni wachezaji bora na wenye elimu bora ya mpira.
Wataalamu wanasema inachukua karibia miaka kumi kumpata mchezaji aliyekamilia, na inachukua muda mrefu pia kupata kocha wa kiwango cha juu.
Jim Hill aliwahi kusema,” mchezaji mpira hakuzaliwa ila mchezaji mpira anatengenezwa kama ilivyo pia kwa makocha”, hivyo kwa upande wangu tatizo la mpira wetu linaenda mbali zaidi, hasa kwenye mizizi ya soka letu na hapo swala kubwa na la kujiuliza ni vipi tunaweza kuwafunza vijana wetu? kwa jinsi gani hasa tunaweza kuzalisha wanasoka bora ambao wanaweza kushindana katika level ya kimataifa?
Mifumo hii ya kuzalisha wanasoka vijana inahitaji kurutubishwa mara kwa mara, inahitaji uangalizi wa hali ya juu. Pia inahitaji kufanyiwa mabadiliko kila baada ya miaka michache kwakwa kuweka mawazo mapya na mbinu mpya bora na za kisasa za ufundishaji kwani mpira kila siku unabadilika na kuwa wa kisasa zaidi.
Tanzania tumefeli kabisa kufanya hivyo kwa miongo kadhaa iliyopita. Mara kadhaa kweli tunakuwa tunapata wachezaji wazuri lakini mabadiliko ya muhimu kwenye mpira wetu bado hayajafanyika, mfumo wa kupata wachezaji wa timu zetu kwa kutumia mpira wa mtaani ni wa kizamani na haufanyi kazi katika ulimwengu wa sasa.
Mpaka sasa umetufanya tuwe hatuna wachezaji waliotengenezwa kifundi, kielimu na hata namna ya kuishi kama wachezaji wa kulipwa na kufika viwango vya kimataifa.
Umefika wakati sasa tuweke pembeni usanii wetu, siasa zetu na ubabaishaji katika mpira wetu wa bongo. Zile danganya toto na mipango ya kupiga pesa ife, tuwekeze kwa ajili ya kizazi kijacho.
Mabdiliko hayo yazingatie na yawe alama na faslsafa mpya ya soka la taifa letu kuanzia ngazi ya taifa, makocha, wachezaji, na washabiki tukubali kwamba tunakwenda kubadili mfumo mzima wa soka la taifa letu mpira unakosa ubora wa kutosha na wala sio kwamba unakosa mafanikio ya kimataifa.
Tusahau Chan 2015, tusahau world cup 2018, tusahau vilabu vyetu kushinda makombe ya kimataifa, hakuna mafanikio ya mzaha tutakayopata na tufikie mahala tuache kudanganyana wenyewe.
Wasalaaam. mwandishi wa makalaa hii anajulikana kwa jina la Abuu Hozza unaweza kunipata kwa facebook au namba ya ya simu ya 0759422148 kwa maoni na ushauri.
0 comments:
Post a Comment