Searching...
Image and video hosting by TinyPic
3 January 2015
Saturday, January 03, 2015

Mapinduzi Cup: Simba mzigoni leo.


Na  Samuel Samuel

Mwaka 1988 Simba SC ilipata matokeo mabovu sana almanusura ishuke daraja. Sababu ya kipindi kile na kinachoendelea sasa vinashabihana kwa ukaribu. 

Mwaka ule walitaka kushuka darajakutokana na uongozi kugawanyika na wachezaji kukosa ari na nguvu ya kuitumikia klabu yao. 

 Hakuna tofauti na kinachoendelea hivi sasa. Duru za uchunguzi zinaonesha hakuna umoja wa viongozi na hata ndani ya wachezaji kuna mpasuko mkubwa. Tazama ujaji wa timu hiyo mjini Zanzibar. Wapo wachezaji waliokuja kwa ndege na wengine boti. 

Hii inaua umoja na mshikamano wa wachezaji. Wapo mashabiki na baadhi ya viongozi walio laani kutimuliwa kwa kocha Patrick Phiri. 

Sasa Simba Leo wakiwa bado kwenye kiza hicho wanajitupa uwanjani kupambana na moja ya timu nzuri mjini Zanzibar ya Mafunzo FC Benchi la ufundi la Simba SC litakuwa chini ya kocha wao mpya ndugu Gorani Korpunovic . 

Huyu kocha bado ni mgeni hivyo bado hajaijua timu hiyo vizuri hivyo tuna amini baadhi ya viongozi na wachezaji nguli kama Ivo Mapunda, Cholo na Kisiga watamsaidia kuipanga timu hiyo. Hiyo inatokana na kumtimua pia kocha msaidizi Matola. 

Ukiitazama Mafunzo inayotumia soka la kasi na pasi fupi fupi basi hakuna tofauti sana na wekundu hao wa Msimbazi. Kukosekana kwa Mganda Emanuel Okwi na kiwango cha chini cha mshambuliaji wao Danny Sserunkuma kama bado hawajavifanyia kazi vitaigharimu timu hiyo. 

Simba inahitaji umoja na mshikamano kama kweli wanalihitaji kombe hilo.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!