Searching...
Image and video hosting by TinyPic
4 August 2014
Monday, August 04, 2014

Barua ndefu kwa TFF: Sehemu ya pili.


 

 Na Abuu Hozza
 0759422148

 

TFF hawana budi kugeuka sasa na kuwekeza kwenye mfumo mzima wa soka letu hasa katika nyanja za soka la vijana, kuliko kuendelea kutilia mkazo Ligi kuu ambayo sasa ni taasisi huru inayoendeshwa na chombo chake binafsi. 

TFF wanapaswa sasa kukomaa hasa na mfumo wa mzima wa mpira wa nchi hii badala ya Ligi ambayo asilimia kubwa inaaendeshwa kwa maslahi ya wenye vilabu vyao.

 Karibia kila taifa utakalolitaja lillofanikiwa kisoka limefanya juhudi za dhati na mipango imara, kiufupi ni mapinduzi ya kisoka kuanzia nchi za Afrika kama Ghana, Cape Verde, Algeria, Ethiopia na Nigeria, nchi za Ulaya kama Ujerumani, Ubelgiji, Craotia, Hispania na nchi kadhaa za Amarica kama Columbia, Costa Rica na Mexico kote wanafanya vizuri baada ya kuacha kukumbatia ubabaishaji na kufanya mambo kisayansi.

 Bert Vogts akiwa mkurugenzi wa ufundi wa shirikisho la soka la Ujerumani, alitengeneza mabadiliko ya mfumo wa elimu ambao ulitoa nafasi ya kuibuliwa kwa vipaji vya soka la vijana, kupitia mpango wake huo shirikisho la soka la ujerumani lilisaidia kwa kutengeneza vituo bora 390 vya soka la vijana nchi ambavyo vyote vilikuwa vikongozwa na walimu waliofikia vigezo bora vya ufundishaji.

 leo hii Ujerumani ni nchi ambayo shule zake za mpira zinazalisha wachezaji vijana wengi zaidi kuliko hata mahitaji yao ya timu ya taifa na vilabu vyake. Mpaka sasa tayari wana vijana zaidi ya 40 ambao wamezaliwa mwaka 1995 na 1996 wenye namba za kudumu katika vilabu vikubwa vinavyocheza ligi ya Bundesliga.

 TFF hapa wana haja ya kutoa nafasi au hata kuajiri wataalamu waliobobea katika masuala ya kiufundi na mipango na sio kutoa nafasi kwa watu kwa kigezo cha kuwa mchezaji wa zamani au kocha mstaafu bila ya kuwa na mipango, elimu, upeo na utashi wa kutengeneza mfumo imara.

 Mpira wetu mpaka sasa umekosa falsafa yake inayojulikana achilia mbali mipango ya muda mrefu, wakati leo hii kila mtu akiiga falsafa ya tik tak(mpira wa pasi fupi fupi na haraka) ya Hispania , Wajerumani wao walikuwa wakiiboresha staili hii ili kupata yao. Fasalsafa Watanzania ya mpira haijulikani na wala hatujajua mpaka sasa kama tunahitaji kuwa nayo.

 Ni muhimu pia kuwa na falsafa yetu ya mpira ambayo itatatufanya na sisi tutambulike Afrika na hata dunia nzima ambayo hata wachezaji wetu watatengenezwa kupitia faslsafa hiyo. 


Kwa sasa kila mtu wazo lake ni kushiriki mashindano makubwa kama Mataifa ya Afrika au Kombe la Dunia lakini kila mmoja wetu kichwani mwake hana wazo la namna gani tunaweza kufika huko.

Tunafanya mchakato kila siku wa kuendelea kushindwa badala ya kubuni imfumo itakayotupatia mafanikio. Tumekuwa magwiji wa kutafuta mchawi kila siku kama sio kocha basi jua jumba bovu litamwangukia mchezaji. 


Tulikuwa tukimlalamikia Samatta hafanyi vizuri akiwa timu ya taifa, akaja Kaseja tukalalama aachwe kiwango kimeisha, Ngassa nae kachuja, Chuji umri umeenda, Kannavaro hana akili ya mpira, sasa tunadai Yondani nae anatumia baadhi ya vitu.


Sehemu ya tatu na ya mwisho inafuata hivi punde....usikose!!





0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!