Searching...
Image and video hosting by TinyPic
4 February 2017
Saturday, February 04, 2017

'SIMU YA GUARDIOLA ILINIFANYA NIJIUNGE NA CITY'- GABRIEL JESUS


Na FLORENCE GR

Mchezaji wa manchester city Gabriel Jesus amefunguka na kusema kuwa simu aliyopigiwa na Pep Guardiola ndio iliyomshawishi mbrazili huyo kujiunga na matajiri hao wa jiji la Manchester.

Akiongelea swala hilo kupitia mndao wa kbalu ya city Jesus alisema kuwa 'nilichukua uamuzi wa kujiunga na city kutoakana na simu aliyonipigia Pep Guardiola' Aliendelea kusema kuwa ' Alinipia, akaongea na mimi kuhusu mipango yake mbalimbali na kunieleza kuwa na mimi naenda kuwa sehemu muhimu ya mipango hiyo'.

'Nilihisi furaha sana. Heshima ya jezi ya manchester city ni muhimu sana, nimekuwa nikiangalia na kuifatilia ligi kuu ,na hizo nni sababu zilizofanya nichukue uamuzi huu'.

Jesus amesema kuwa mshikamano alionao na kocha wake utamsaidia sana kwani wote wawili wanaupendo sawa juu ya mchezo wa mpira.

'Ni kichaa wa mpira kama mimi , masaa 24 ya siku kama sijaenda mazoezi au kucheza mechi basi takuwa naangalia mpira kwenye TV au kitu chochote kinachoendana na mpira kwenye simu yangu au wapinzani wetu tunaokwenda kucheza nao mechi ijayo'.

Alielezea kuwa kwa kipindi kifupi alichokaa Man city amegungua kuwa Pep ni mtu mzuri sana na anastahili kushinda mataji yote aliyoshinda kwenye 'carrier' yake ya ukocha.

Gabriel Jesus ana miaka 19 na alijiunga na Manchester city kwenye kipindi cha dirisha dogo la usajili mwezi January akitokea klabu ya Palmeiras ya nchini brazil na amefanikiwa kuonyesha kiwango kizuri tangu alipojiunga na city ambapo tayari ameshafunga na kutoa pasi ya goli katika mechi chache alizocheza.


0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!