TRANSFER ZILIZOTEKA VYOMBO VYA HABARI ULAYA
Na FLORENCE GR
Dirisha la usajili linatarajiwa kufungwa jumanne majira ya saa 00:00 huku timu mbalimbali brani ulaya likiwa katika mawindo ya mwisho mwisho kuhakikisha wanaimarisha vikosi vyao kwa ajili ushiriki wao katika ligi mbalimbali wanazoshiriki.
Zifuatazo ni "transfers' mbalimbali zilizogongwa vichwa vya habari barani ulaya;
Oscar kutoka chelsea kwenda Shanghai SIPG
Mchezaji huyo raia wa Brazil alijiunga na chelsea kutoka Internacional kwa kiasi cha euro million 25 mwaka 2012 na amefanikiwa kuifungia chelsea magoli 38 katika mechi 203 aliyoichezea klabu hiyo.
Oscar ambae hakuwa anapata nafasi chini ya kocha Antonio Conte alijiunga na kocha wake wa zamani Andre Villa -Boas kwa kitita cha euro million 52 na kufanya kuwa mchezaji alisajiliwa kwa pesa nyingi katika dirisha dogo hili la majira ya baridi .
Katika kipindi cha miaka minne na nusu katika klabu ya chelsea oscar amefanikiwa kushinda ligi kuu uingereza mara moja, europa ligi na kombe la ligi mara moja.
Carlos Tevez kutoka Boca Junior kwenda Shanghai Shenua
Muargentina huyo mwenye umri wa miaka 32 alijiunga na timu hiyo kwa kitita cha euro million 40 huku akitarajiwa kulipwa kiasi cha 310,000 kwa wiki na kuwa mwanasoka anayelipwa pesa nyingi kuliko wote.
Tevez alicheza EPL kwa muda wa miaka saba huku akifanikiwa kuchukua ubingwa na klabu zote mbili za jiji la Manchester,pia alifanikiwa kubebwa ubingwa wa ulaya akiwa na manchester united mwaka 2008 kabla ya kwenda Juventus na kufanikiwa kuchukua ubingwa wa italia mara mbili.
John Obi Mikel kutoka chelsea kwenda Tianjin TEDA
Mchezaji huyo raia wa Nigeria alitangaza kuondoka katika klabu ya chelsea kupitia mtandao wa kijamii hivyo kuhitimisha miaka yake 10 kakika klau jiyo huku akifanikiwakuichezea jumla ya mechi 374 klabu hiyo.
Obi alijiunga na chelsea akiwa na umri wa miaka 19 kutoka klabu ya Lyn inayoshiriki ligi kuu nchini Norway mwaka 2006 alikuwa katika wakati mgumu wa kupata namba chini ya Conte huku akifanikiwa kucheza mchezo mmoja tu.
Mikel amefanikiwa kushinda mataji 11 akiwa na chelsea ikiwemo kombe la mabingwa barani ulaya mwaka 2012.
Obi alijiunga na Tianjin kwa kiasi ambacho hakikuwekwa wazi.
Dimitri Payet kutoka West ham united kwenda Marseille
Mchezaji huyo raia wa Ufaransa alizua kizazaa pale alipogoma kuichezea klabu akishinikiza kuondoka kwenye klabu hiyo baada ya kuhitajiwa na timu mbalimbali.
Mfaransa huyo alikuwa katika kiwango cha hali ya juu hali iliyopelekea klabu mbalimbali kama manchester united kuonyesha nia ya kutaka kumsajili hivyo kuomba kuondoka klabuni hapo aambapo timu hiyo kufanya vibaya katika ligi kuu nchini uingereza.
Payet alikamilisha uhamisho wake na kurudi katika klabu yake ya zamani ya Marseille inashiriki ligi kuu nchini ufaransa kwa kiasi cha euro 25 na kusaini mkataba wa miaka minne na kuacha simanzi kwa mashabiki wa west ham.
0 comments:
Post a Comment