Searching...
Image and video hosting by TinyPic
27 November 2014
Thursday, November 27, 2014

Ballon D'or kupewa mchezaji wa Ujerumani.


Rais wa Uefa, Michel Platini ameibuka na kusema mshindi wa mchezaji bora wa Dunia mwaka huu anatakiwa kutoka kwenye kikosi cha mabingwa wa Dunia, timu ya taifa ya Ujerumani. Ujerumani katika kinyang'anyiro hicho, inawakilishwa na wachezaji watano.

Kiungo Ton Kroos ambaye anakipiga na Real Madrid kwa sasa, anaungana na wachezaji wanne kutoka klabu ya Bayern Munich Philipp Lahm, Bastian Schweinsteiger, Manuel Neuer, Thomas Muller na Mario Gotze. 

Katika orodha hiyo ya awali kama kawaida, imesheheni majina ya Lionel Messi na Christiano Ronaldo ambao ni gumzo kwa ubora wao ndani ya miaka mitano mfululizo ya hivi karibuni.

Platini pia aliwahi kusema mwaka 2010 kuwa, angependa kuona mchezaji bora wa Dunia akitoka kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Hispania ambao ndiyo walikuwa mabingwa wa Dunia lakini, mambo yalikuwa tofauti baada ya tuzo hiyo kuchukuliwa na Lionel Messi wa Argentina.

Upigaji wa kura umekamilika tangu tarehe 23 Novemba na mwezi ujoa, FIFA watatangaza majina ya wachezaji watatu ambao wataingia katika Kapeti jekundi mwezi January kwenye sherehe za kumtangaza mchezaji ambaye atakuwa amechaguliwa kwa kura za Makocha, Manahodha wa nchi wanachama wa FIFA na wawakilishi wengine waliopendekezwa na FIFA.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!