Searching...
Image and video hosting by TinyPic
28 January 2015
Wednesday, January 28, 2015

Real Madrid kubadili jina la uwanja.


Na Chikoti Cico
Klabu ya Real Madrid inatarajiwa kubadilisha jina la uwanja wake wa Santiago Bernabeu na kuitwa Abu Dhabi Bernabue kama sehemu ya dili la pauni milioni 15 kwa mwaka kati ya Real Madrid na serikali ya Abu Dhabi kupitia kampuni ya cepsa ambayo inamilikiwa na IPIC (International Petroleum Investment Company) na ambayo inamilikiwa na serikali ya Abu Dhabi.
Cepsa ni kampuni ya nne kati ya makampuni yanayoingiza kipato kikubwa nchini Hispania huku kampuni ya IPIC ambayo iliundwa mwaka 1984 ikiwa imewekeza kwenye makampuni mengine 18 yanayoongoza ndani ya nishati na sekta zinahusiana na nishati duniani kote.
Mwezi Novemba mwaka jana wakati Madrid walipotangaza mkataba wa miaka mitatu kati yao na IPIC raisi Florentino Perez alidakwa na kamera akisema “uwanja utaitwa “IPIC ama Cespa, vyovyote wanavyotaka”. Kutokana na ripoti ya AS wadhamini hao wamekubali jina la “Abu Dhabi Bernabeu”.
Kubadilishwa kwa jina la uwanja wa Santiago Bernabeu hautafanyika mpaka hapo uwanja huo utakapofanyiwa marekebisho mapya na kwasasa klabu ya Real Madrid inamalizia mambo ya fedha kwaajili ya kuuendeleza uwanja huo.
Klabu ya Madrid ambayo karibuni imetajwa kuingiza kiasi cha pauni milioni 459.5 kama mapato kwa msimu wa mwaka 2013/2014 itaingiza fedha zaidi kwa kubadilisha jina la uwanja huo kitu ambacho kinatarajiwa kuwakasirisha mashabiki wa klabu hiyo kubwa duniani.
Uwanja wa Santiago Bernabeu ulifunguliwa mwaka 1947 na kupewa jina la Mwenyekiti wa zamani wa klabu hiyo Santiago Bernabeu Yeste na umeweza kuwa mwenyeji wa fainali nne za kombe la Ulaya na fainali ya kombe la Dunia kwa maka 1982.
Uwekezaji wa pauni milioni 300 wa Abu Dhabi utakuwa ni dili kubwa sana kwa klabu hiyo katika historia na utasaidia kutoa fedha kwaajili ya kuendeleza uwanja huo wa zamani kitu ambacho kitaifanya klabu hiyo kuwa mbele ya wapinzani wao klabu ya Barcelona ambayo wanatarajiwa kuupitia mkataba wao wa pauni milioni 123.4 na kampuni ya Qatar Sports ambao utaisha muda wake mwaka kesho na kuna uhakika kwamba utaongezeka.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!