Na FLORENCE GR
Hatimaye mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Arsenal, Manchester city, Tottenham na Crystal palace Emmauel Adebayor amefanikiwa kujiunga na klabu ya Istanbul Basaksehir inayoshiriki ligi kuu nchini Uturuki kama mchezaji huru.
Raia huyo wa Togo mwenye umri wa miaka 32 alikuwa huru tangu alipoachana na klabu yake ya Crystal palace kwenye kipindi cha majira ya joto mwaka jana.
Adebayor ambaye amesaini mkataba wa miezi 18 kuitumikia klabu hiyo mara baada ya kufanikiwa kufaulu vipimo vya afya vilivyofanyika jumanne katika Hospital ya chuo cha Medipol Mega iliyoko mjini Istanbul.
Katika mkataba huo Basaksehir wameweka kipengele cha endapo kiwango cha Adebayor kitapanda na kuisaidia timu hiyo kufunzu michuano ya Europa au Klabu bingwa ulaya msimu ujao basi mchezaji huyo atapata ongezeko la bonusi katika mkataba wake wa sasa.
Basaksehir ambao wanashika nafasi ya pili katika msimamo wa ligi kuu nchini humo nyuma ya mabingwa watetezi Besiktas kwa tofauti ya pointi mbili na endapo wakishinda kombe hilo ilakuwa timu ya sita kuchukua kombe hilo ikiungana na Besiktas, Bursaspor, Fenerbahce, Galatasaray naTrabzonspor.
0 comments:
Post a Comment