Searching...
Image and video hosting by TinyPic
27 August 2014
Wednesday, August 27, 2014

Arsenal vs Besiktas saa 3:45 usiku wa leo.



 Na Oscar Oscar Jr

London kaskazini usiku wa leo patakuwa hapatoshi kuelekea mechi ya marudiano ya kufuzu kwa hatua ya makundi Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya Arsenal watakapokabiliana na Besiktas, Gunners wakiwa hawajawahi kufungwa na timu ya Uturuki nyumbani. 

Pamoja na kuwa na rekodi nzuri kwenye hatua hii ya awali kwenye klabu bingwa Ulaya, Arsenal haijaanza kwa makeke msimu mpya wa ligi kuu Uingereza. 

Katika mechi mbili walizocheza pamoja na kujikusanyia alama nne baada ya kutoka sare mchezo mmoja na kushinda mmoja, bado timu haijaonyesha mchezo wa kuvutia.

Hii mechi ya 14 sasa chini ya kocha Arsene Wenger akiwa na klabu hiyo ya London akishiriki michezo hii ya awali kabla ya hatua ya makundi na katika mechi 12 ya misimu ya nyuma, Arsenal alishinda zote lakini msimu huu, alishindwa kupata ushindi ugenini dhidi ya Besiktas ambao leo watakuwa Emirates.

Arsenal watamkosa Aaron Ramsey ambaye alipewa kadi nyekundu mechi ya kwanza, Arteta, Giroud na Gibbs wote ni majeruhi. Kuwakosa nyota hao ni pigo kubwa kwa washika Bunduki hao wa London. 

Leo ni siku ambayo Alexies Sanchez na Mesut Ozil wanatakiwa kuipigania timu yao na kuonyesha thamani ya pesa lukuki zilizotumika kuwasajili. Ozil hakuwa vizuri sana msimu wake wa kwanza huku Sanchez nae akishindwa kung'aa kwenye mechi chache ambazo amekuwa na Arsenal.

 
Besiktas hawajashindwa katika mechi zao tatu za hivi karibuni za Ligi ya mabingwa Ulaya na ushindi wao wa kustua ulikuwa pale Old Trafford walipomfunga Manchester United FC 1-0 hatua ya makundi 2009/10 na 2003 waliwahi kutua London na kumfunga Chelsea 2-0.

Kiungo nguzo wa Besiktas Atiba Hutchinson ambaye alikosa mchezo wa awali, leo atakuwa fiti kuwavaa Gunners huku mshambuliaji wa zamani wa Chelsea, Demba Ba atakuwa akiongoza safu ya ushambuliaji ya timu hiyo ya Uturuki.

Mustapha Pektemek na Ocay Sahan ni viungo washambuliaji walioisumbua sana Arsenal kwenye mchezo wa awali na leo kocha Slaven Bilic, ametamba kuwaanzisha. 

Arsenal wanamapungufu makubwa leo kwenye safu ya kiungo na ushambuliaji na huenda Alex Sanchez au Joel Campbell mmoja akaanza kama mshambuliaji.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!