Searching...
Image and video hosting by TinyPic
27 October 2014
Monday, October 27, 2014

Kocha Mwambusi na tafsiri ya neno "Uzalendo"



 Na Samuel Samuel

Wakati bundi wa mkosi akionekana kutua kwenye kambi ya Mbeya City msimu huu, malaika wa bahati anaonekana kuzidi kutanua mbawa zake ndani ya Mtibwa Sugar. 

Mwambusi na baadhi ya viongozi wa mbeya city inaonekana dhana ya neno "uzalendo" katika soka, hawakulielewa vizuri. Tunafahamu mnaijenga timu hiyo kutokana na vijana halisi wa mkoa huo mkiwa na imani kubwa ya kujituma, kujitoa na kuitetea timu ya mkoa wao. 

Ni sawa na pia ni jambo zuri katika kuuendeleza mkoa huo kisoka. Lakini hebu tuangalie dhana ya uzalendo katika kiwango cha kimataifa. Ikumbukwe Mbeya City imeshiriki mwaka huu michuano mipya ya CECAFA iliyofanyika kule nchini Sudani . 

Meneja yoyote wa timu akisharidhika na mchezaji katika kipaji chake, nidhamu, afya, uzalendo wa kukitendea haki kipaji chake popote pale anapocheza, basi atasajiliwa ili mradi tu sharia zinaruhusu. 

Mwambusi amemsajili wachezaji wachache nje ya mkoa huo lakini kwa soka ambalo walicheza msimu uliopita, ilimpasa kutafuta wachezaji wakuipa nguvu timu hiyo. 

Mkoa Mbeya unasifika kwa vipaji lakini huwezi kuwa na chanzo kimoja tu cha kukupatia mchezaji wa ligi kuu. Wazungu na academies zao lakini wanakuja Afrika kutafuta vipaji. 

Mwaka Jana timu hiyo ilimaliza nafasi ya tatu , sasa tulitarajia mwaka huu ingekuja na moto mkali kuhitaji ubingwa wa nchi hii ambao unashikiliwa na Azam  lakini, imeanza kutupa mashaka timu hiyo. 

Mpaka sasa imeshinda mchezo mmoja tu. Imefungwa mara mbili na kutoa droo mbili. Mwambusi unahitaji wachezaji wanne wenye kiwango cha kimataifa kuwapa changamoto wazawa wa timu hiyo. 

Wakati Azam  inaibuka ilikuwa inapewa onyo na wanaojiita watu wa mpira nchi hii . Azam ilionywa isichukue mchezaji Simba na Yanga ili isijifunge kwenye siasa za vilabu hivyo vikongwe zaidi nchini lakini ilikuwa ni upotoshwaji mkubwa. 

 Azam ilianza kusajili toka vilabu hivyo na imezidi kung'ara kwenye ligi. Kavumbagu analipa thamani ya usajili huo. Ifike wakati tuwe tunatafsiri sahihi ya neno uzalendo.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!