Balotelli anatakiwa kuisaidia Liverpool
Na Oscar Oscar Jr
Baada ya kumaliza kwenye nafasi ya pili msimu uliopita, Liverpool wamejitosa sokoni kimarisha kikosi chao na moja ya kati ya watu waliotua kikosini mwao ni Super Mario Balotelli.
Mario Balotelli amefurahi kurudi kucheza ligi ya Premier ya Uingereza baada ya kukamilisha uhamisho wake kutoka AC Milan na kujiunga na Liverpool kwa ada ya pauni milioni 16.
Balotelli aliondoka Uingereza Januari 2013 na kwenda kujiunga na klabu ya Ac Millan ambapo hakuwa na msimu mzuri sana kwa sababu timu hiyo haikuweza kufanya vizuri kwenye michuano ya ligi kuu na ile ya klabu bingwa Ulaya.
Baada ya kukamilisha kujiunga na Liverpool kwa mkataba wa miaka mitatu ambao una chaguo la kuongezewa mwaka mwingine na ajira ya pauni 90,000 kila wiki, Balotelli hakuchukua muda kuelezea kufurahishwa kwake na kitendo cha kurejea Uingereza.
"Nafurahi kurudi kwani kuondoka Uingereza kulikuwa ni makosa. Nilitaka kwenda Italia lakini ni kagundua ni makosa makubwa"
Balotelli ni mtu ambaye haeleweki kutokana na tabia zake za utovu wa nidhamu. Amejiunga na Liverpool ambayo imeondokewa na mfungaji wake bora Luiz Suarez aliyejiunga na klabu ya Barcelona hivyo anatakiwa kutulia na kuisaidia timu.
0 comments:
Post a Comment