Searching...
Image and video hosting by TinyPic
27 October 2014
Monday, October 27, 2014

Mambo magumu kwa kocha Juma Mwambusi.


Na Oscar Oscar Jr

Timu ya Mbeya City ambayo msimu uliopita ilikuwa gumzo kutokana na uwezo mkubwa na ushindani walio onyesha, msimu huu wamekuwa na mwanzo mbaya hasa baada ya kushindwa kutumia vema  uwanja wa nyumbani, Sokoine Mbeya na kujikuta wakipigwa na wageni timu za Azam na Mtibwa Sugar.

Bado tatizo la ushambuliaji lililokuwa linawasumbua Mbeya City msimu uliopita, linaonekana kuendelee pia msimu huu. Mpaka sasa, Mbeya City ndiyo timu ambayo ina safu mbovu ya ushambuliaji kuliko timu nyingine yoyote wakiwa na goli moja pekee lililopatikana kwa mkwaju wa Penalty.

Umakini pia wa mabeki wa kocha Juma Mwambusi, unaonekana kusua sua kwa sababu aina ya magoli wanayofungwa, yapo amabyo wangeweza kuyaepuka. 

Mechi ijayo watalazimika kwenda mkoani Tanga kucheza na Mgambo JKT, mchezo ambao utakuwa na presha kubwa sana kwa kocha na wachezaji.

Baada ya mechi ya jana kumalizika na kupata  kichapo cha mabao 2-0, mashabiki wa Mbeya City walianza vurugu huku kukiwa na habari ambazo sio rasmi kuwa, kocha Juma Mwambusi alilazimika kutoka uwanjani hapo usiku kwa madai ya kuwepo mashabiki waliokuwa wanataka kumfanyia vurugu kocha huyo ambaye msimu uliopita, alitangazwa kama kocha bora ligi kuu Tanzania bara.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!