Alex Song ndani ya Anfield
Na Oscar Oscar Jr
Meneja wa Liverpool, Brendan Rodgers anaifahamu vema kazi yake na sasa anataka kuithibitishia dunia kwamba yupo tayari kupambana kwenye ligi kuu nchini Uingereza na barani Ulaya ambapo pamoja na timu nyingine, atapambana na mabingwa watetezi wa taji la Ulaya Real Madrid kwenye hatua ya makundi.
Rogers amejipanga kuivamia kambi ya Barcelona na kumnasa kiungo Alex Song ambaye ameshindwa kupata nafasi kwenye kikosi hicho ambacho kwa sasa kina nolewa na kocha Luiz Henrique. Adres Iniesta, Ivan Rakitic ni baadhi ya wachezaji wanaomfanya Song akose nafasi.
Liverpool inaonekana kupwaya hasa kwenye safu ya kiungo mkabaji ambapo amekuwa akicheza nahodha Steven Gerrard. Gerrard alifanya vizuri katika nafasi hiyo msimu uliopita lakini ni wazi kuwa anahitajika mtu mwingine wa kumpunguzia majukumu na kuleta ufanisi zaidi.
Liverpool waliruhusu kufungwa mabao 50 msimu uliopita na moja ya sababu ilikuwa ni kukosa kiungo mkabaji ambaye atasaidia kuwalinda walinzi wake. Alex Song bila shaka anaiweza kazi hiyo na kikubwa zaidi, ni mchezaji anayeifahamu vema ligi kuu ya Uingereza.
Tatizo ni kuwa Liverpool wanataka kukamilisha makubaliano ya msimu mmoja kwa mkopo lakini Barca hawataki kwa sababu wanania ya kumuuza moja kwa moja kwa pauni milioni 10.
0 comments:
Post a Comment