Iniesta asema ni zaidi ya pointi 3 pale Bernabeu.
Na Oscar Oscar Jr
Kiungo na Nahodha wa klabu ya Barcelona, Andres Iniesta amesema kuwa, mechi yao ya Jumamosi hii dhidi ya Real Madrid ni zaidi ya Pointi tatu.
Kocha wa Barcelona, Luis Enrique ameweza kuiongoza Barcelona kwenye michezo nane msimu huu ya La Liga pasipo kuruhusu hata bao moja kutinga kwenye wavu wao.
Barcelona wanakwenda kwenye mchezo huo wakiwa na alama 22 huku wakifunga magoli 22 na kuongoza ligi. Iniesta ameeleza kuwa, unapopata ushindi kwenye mchezo wa El-Classico unajenga hali ya kujiamini na kuendelea kufanya vizuri.
Kiungo huyo ana amini kuwa timu yake ina uwezo wa kushinda mechi hiyo ingawa imekiri kuwa haitokuwa rahisi.
Mchezaji bora wa dunia, Christiano Ronaldo amelalamika kuwa Real Madrid hawajapata muda mwingi wa kupumzika kutokana na wao kucheza mchezo wa Uefa siku ya Jumatano huku wapinzani wao, Barcelona wakicheza siku ya jumanne na kupata siku moja ya ziada ya kujiandaa na El-Classico.
Akijibu hilo Iniesta amesema, Real Madrid wanatakiwa kujiandaa tu kwani hata wao wametoka kucheza muda sio mrefu hivyo hadhani kama madai ya wao kupata muda wa masaa 24 zaidi ya kujiandaa kuliko Real Madrid kama yanaweza kuwa ndiyo chanzo cha timu kupata matokeo.
Katika michuano ya Ulaya, Barcelona ilipata ushindi wa magoli 3-1 dhidi ya Ajax huku Real Madrid wakishinda, magoli 3-0 dhidi ya Liverpool.
Timu hizi zitakutana kwenye mechi ya kwanza ya El-Classico msimu huu jumamosi hii kwenye dimba la Bernabeu.
0 comments:
Post a Comment