Na Chicoti (Cico cicod)
0755 700 076
Alonso tayari amejiunga na klabu ya Bayern Munich Baada ya kuichezea Real Madrid kwa zaidi ya miaka 4 hatimaye kiungo wa mhispania Xabi Alonso akaribia kutua Bayern Munich kwa ada ya paundi milioni 7.5 kuungana na kina Thiago Alcantara na Javier Martinez hii na baada ya kocha Carlo Ancelotti kuonekana kumpa nafasi zaidi mjerumani Toni Kroos katika sehemu ya kiungo ya Madrid.
Katika umri wa miaka 32 Alonso ameonyesha kuhitaji changamoto mpya hasa ikizingatiwa usajili wa Kroos mapema mwezi wa 7 kutoka Bayern kwenda Madrid kwa paundi milioni 24 kumefanya nafasi ya Alonso kwenye kikosi cha kocha Ancelot kuwa ndogo.
Bayern Munich ambao walianza kufungua pazia la ligi ya Ujerumani maarufu kama Bundesliga wiki iliyopita dhidi ya Wolfsburg bila ya viungo Bastian Schweinsteiger, Thiago Alcantara na Javi Martinez ambao ni majeruhi licha ya kushinda kwa magoli 2-1, wanatarajia kwa kumsajili Alonso itasaidia kuongeza makali ya safu yake ya kiungo chini ya kocha Pepe Guadiola.
Baada ya karibuni kutangaza kustaafu kuichezea timu ya tafa ya Hispania Alonso ameamua kujiunga na mabingwa wa Ujerumani Bayern Munich ili kupata nafasi ya kuendelea kucheza hasa ikizingatiwa Madrid wana wachezaji kama Kroos na Modric ambayo wanatengenza sehemu ya kiungo ya kocha wa Madrid Carlo Ancelotti.
0 comments:
Post a Comment