Eto'o na Lukaku kuimaliza Chelsea?
Na Oscar Oscar Jr
Nahodha wa Chelsea, John Terry, amewaonya wenzake kuelekea mpambano wa kukata na shoka ambao utawakutanisha na nyota wa zamani wa timu hiyo ambao kwa sasa wanakipiga na Everton.
Terry anajaribu kuwatahadharisha wenzie kwani Samuel Eto'o na Romeru Lukaku wanataka kumuaibisha Mourinho.
Pamoja na kuonyesha uwezo mkubwa wa kufumania nyavu za timu pinzania akiwa kwenye timu mbalimbali kwa mkopo, bado Lukaku hakuweza kuaminiwa na kocha Mourinho ambaye msimu uliopita mshambuliaji wake mwenye mabao mengi aikuwa ni Eto'o pekee akifunga mabao 12 huku Torres na Demba Ba wakifunga machache kila mmoja.
Kuna habari kuwa nyota hao wawili wa zamani wa Chelsea, wamepanga kuisambaratisha timu hiyo pale zitakapokutana kesho kwenye dimba la Goodison Park. Terry amesema wachezaji wenzie ni lazima kila mtu atimize wajibu wake na kuhakikisha wanaibuka na ushindi.
Lukaku na Samuel Eto'o watakutana kwa mara ya kwanza na timu hiyo waliowahi kuitumikia huku wakifahamu wazi kuwa Mourinho nae amejipanga kuhakikisha anaendeleza ushindi licha ya kumkosa Diego Costa ambaye ameumia na kuna taarifa kuwa atakaa nje kwa takribani majuma sita.
0 comments:
Post a Comment