Mats Hummels ameikatia tamaa Borussia Dortimund
Na Oscar Oscar Jr
Beki wa kimataifa wa Ujerumani na klabu ya Borussia Dortimund, Mats Hummels, ameibuka na kudai kuwa kuna uwezekano mkubwa msimu huu wasiweze kufanikisha malengo waliojiwekea mwanzoni mwa msimu kufuatia matokeo mabovu ya timu yao.
Pamoja na kuwa mpinzani wa karibu wa Bayern Munich, Dortmund msimu huu wanaonekana kuchechemea baada ya kupoteza mchezo wa nne mfululizo huku wakiwa uwanja wa nyumbani weekend iliyopita.
Vijana hao wa kocha Jurgen Klopp, wanashika nafasi ya 15 kwa sasa kwenye msimamo wa bundesliga baada ya kushuka dimbani mara tisa na kuambulia alama saba pekee.
Kinyume na matarajio ya wengi, timu hiyo inaonekana kufanya vizuri sana kwenye michuano ya Uefa ambapo mpaka sasa, wao ndiyo wanaongoza kundi lao wakiwa na alama tisa kutokana na kushinda michezo yao yote mitatu kwenye hatua ya makundi.
Klabu ya Bayern Munich chini ya kocha Pep Guardiola, wanaongoza ligi hiyo wakiwa na alama 21 na kuwa timu yenye safu bora ya ulinzi kwa kuruhusu nyavu zao kutikiswa mara mbili tu.
Beki huyo ameonekana kukata tamaa ya ubingwa wa Bundesliga hasa baada ya kichapo cha nne mfululizo weekend iliyopita dhidi ya Hannover 96.
0 comments:
Post a Comment