AZAM FC inahaha kila kona kuhakikisha beki Shomari Kapombe anatua katika himaya yao tayari kwa ajili ya kumtumia katika msimu ujao na imeweka mezani ofa ya maana kumnunua beki huyo kutoka AS Cannes ya Ufaransa.
Akizungumza na Mwanaspoti kutoka Ufaransa asubuhi
jana (Ijumaa), wakala wa beki huyo Dennis Kadito alisema, Azam imekuwa
katika jitihada kubwa za kuhakikisha inamsajili mteja wake huyo, ambapo
awali kupitia kwa Yusuf Bakhresa walituma ofa ya Euro 40,000 (Sh milioni
88) ambazo ziligomewa na Wafaransa hao.
Kadito alisema Cannes baada ya kugoma, Azam
waliwatajia kiasi ambacho wanakihitaji ili kumuuza beki huyo ambacho ni
Euro 70,000 (Sh milioni 154) na Yusuf ambaye pia ni wakala wa kuuza
wachezaji alikubali kulipa.
Inadawa kwamba, Azam walikubali kulipa kiasi hicho
baada ya kugundua wameshafanya makosa ya kumshawishi Kapombe avunje
mkataba wake na Cannes na beki huyo tayari ameshawasilisha barua ya
kufanya hivyo tangu Februari 27, mwaka huu.
“Nilipigiwa simu na Yusuf ambaye alitaka kumnunua
Kapombe ili asajiliwe Azam FC kwa kiasi hicho cha Euro elfu 40 lakini
kikakataliwa na Cannes ambako wanataka elfu 70,Yusuf hakukubali akasema
ataangalia jinsi ya kutumia sheria kumpata Kapombe.
“Baadaye Kapombe alituma barua Cannes akitaka
mkataba wake na klabu hiyo uvunjwe, barua hiyo iliandikwa na mchezaji
mwenyewe lakini ukiichunguza kwa makini ni wazi kwamba alipata msaada
kutoka kwa wanasheria,” aliongeza Kadito licha ya kwamba Yusuf
hakupatikana jana kutoa ufafanuzi wa suala hilo.
source:Gazeti la Mwanaspoti.
source:Gazeti la Mwanaspoti.
0 comments:
Post a Comment