WAYNE ROONEY KUIKOSA MECHI YA LEO NA ILE YA BAYERN.
Na Oscar Oscar Jr
+255789784858
Hali ya wasiwasi imetanda kwa mshambuliaji wa Man United Wayne Rooney kuelekea mchezo wa marudiano wa klabu hiyo na Bayern Munich baada ya mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Uingereza kupata tatizo kwenye kidole gumba na kuondolewa kwenye timu itakayo pambana leo na Newcastle United.
Rooney amepatwa na mchubuko kwenye dole gumba lake kipindi cha pili kwenye mchezo ambao ulimalizika kwa sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya mabingwa watetezi Bayern kwenye robo fainali ya ligi ya mabingwa mchezo uliofanyika kwenye dimba la Old Trafford siku ya jumanne.
Ilitarajiwa kuwa Rooney atapona mapema na kuiongoza timu yake kuelekea pale St James' Park, lakini kocha wa Man United David Moyes ameeleza kuwa mshambuliaji huyo bado hajapona na kwa sasa wanampango wa kumfanyia vipimo na uchunguzi zaidi ili kujua kama tatizo limeendelea kwa kiwango gani.
"Wayne alipata mchubuko mbaya kwenye dole gumba," Moyes aliwaambia MUTV siku ya ijumaaon . "Alipatwa na tatizo hilo siku iliyofuata baada ya mchezo ndipo likagundulika.
.
"Kumchezesha au kutomchezesha hiyo sio kitu"
"Ni kweli alipata tatizo kubwa na hilo sio tatizo kwetu tu,hata Bayern nao wanamatatizo kwa hiyo hatutaathirika kwa lolote na tunajipanga kwa hilo kwenye mchezo wetu wa jumatano.
Moyes atalazimika kumuandaa Hernandez na Danny Welback kwa ajili ya mchezo huo kwa sababu tayari mshambuliaji wake tegemeo wa Kidachi,Robin Van Persiea,atakosa mechi hiyo na Rooney naye bado yuko kwenye hati hati ingawa,asilimia ni ndogo sana kwa mshabuliaji huyo kucheza mechi ya Bayern siku ya jumatano.
"
0 comments:
Post a Comment