NIONAVYO MIMI PALE ARSENAL MSIMU HUU.
Ukimuona mtu anaponda usajili wa MESUT OZIL kwenda emirates usipoteze muda kulumbana nae,mwenzio anaona wivu anatamani OZIL angenunuliwa na kocha wake.Bonge moja la usajili ambao wenger kafanya,sio jina kubwa tu bali "a world class player"
Ilipofika jana saa 6 usiku kunahabari ilitoka kwamba ZIDANE amesema usajili wa OZIL kwenda arsenal usitishwe,niliona watu wengi sana wakifurahi kwamba arsenal imemkosa star huyu ambaye ni bingwa wa pass za mwisho.Ilipotimu saa 7 usiku website ya arsenal ilithibitisha kumnasa fundi huyu,wapambe wote wakaenda kulala.
Nje na OZIL,arsenal ilimrudisha mfaransa Methieu Flamini kaka wa dimba la chini ambalo lilionekana kulegea pale arsenal,wenga bado alikuwa na kiu ya kumpata golikipa na amefanikiwa kumnasa mtaliano Emiliano.Flamini atasaidia sana kazaliwa 1984 na Emiliano 1985.
Olivier Giroud is on fire this time, Podolski nadhani watakuwa na kazi moja tu,kupokea pass murua toka kwa JACK10,CARZOLA,OZIL na pale ambapo kila kitu kitashindikana ANKO TOM ataingia nazo mwenyewe na kupasia nyavu.
Jernkison na Sagna wapo kulia,Gibbs na Monreal wapo kushoto.Varmerleen,Conscienly na Martesacker wapo kati na juu yao kuna Ramsey Rambo,Arteta na Flamini kuna sehemu nimesahau?
secszcney,Emiliano na Fabianski wanalinda goli,tafadhali naomba mumtafutia kabinti kazuriiiiii mzeee wenger ili kawe kanamsaidia kufunga zipu ya lile jacket lake maana msimu huu ni kicheko tu kwa kwenda mbele.
0 comments:
Post a Comment