Searching...
Image and video hosting by TinyPic
29 August 2013
Thursday, August 29, 2013

NIONAVYO MIMI KWENDA TIMU KUBWA WAKATI MWINGINE SIO SAHIHI.


Christian Benteke
huyu kijana toka ubelgiji naona sasa ataanza kuogopwa,anamwili mkubwa na anajua kuutumia.Huwezi kucheza na Aston Villa ukaacha kumzungumzia kijana huyu.Nadhani Villa Park ndiyo sehemu yake inayomfaa,anapedwa, na kila mtu yuko nyuma yake.Hatakiwi kuhama,wacha abaki hapo hapo aendelee kututia adabu.


Migel Perez
wengi sana tunamfahamu kama michu,huyu jamaa wa Kihispania unaweza muona kama yuko slow hivi ila shuhughuli yake ni balaa,ukiona anapeleka kale ka mkono kake sikioni,jua kabisa alishaharibu hali ya hewa.Anajua kufunga sana huyu mtu,anakaba,anambio.Hawa ndiyo wanaoifanya EPL izidi kuwa na mvuto.

Tom Hundlestone
huyu ni kijana wa kiingereza na baada ya SPURS kumpata Paulinho,wamemwachia Tom aende Hull city.Tom alipiga mpira mwingi sana alipoingia kutoka bechi mechi na chelsea,Tom hajaanza leo ni fundi sana kama unamfuatilia huyu jamaa.Alikosa nafasi pale white hart lane na kwa sasa nadhani ndiyo muda wake kushaini ndani ya uzi wa Hull city.

Jonjo shelvey
huyu dogo alikuwa pale anfield na hakuweza pata nafasi ya kutosha kwa sababu Dunia nzima inamwangalia Gerrard na Suarez.Amekwenda swansea city na pale nadhani ndo mahala pake.Anapiga faulo zote na mipira ya kufa ipo kwa ajili yake.Kama uliona alichokifanya kwenye mechi na united utakuwa unanielewa vizuri.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!