Searching...
Image and video hosting by TinyPic
3 March 2015
Tuesday, March 03, 2015

Manchester United bado yaumiza kichwa kwa Van Persie






Na Florence George


Klabu ya soka ya Manchester United bado haijafahamu ni muda gani mshambuliaji wake wa kimataifa wa Uholanzi Robin Van Persie atakuwa nje ya uwanja baada ya kupata majeraha ya kifundo cha mguu(Ankle).

Van Persie mwenye umri wa miaka 31amaye alikosekana kwenye ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya Sunderland hatokuwemo katika mchezo wa kesho dhidi ya Newcastle kutokana na majeraha ya kifundo cha mguu aliyoyapata katika kipigo cha magoli 2-1 dhidi ya Swansea City wiki moja iliyopita.

Baada ya mechi dhidi ya Newcastle United ,United itapambana na Arsenal katika kombe la FA,Totenham Hotspur pamoja na Liverpol ambazo mchezaji huyo aliyefunga magoli 10 mpaka sasa anatarajiwa kuzikosa.

Akongea na waandishi wa habari kocha wa United Mholanzi Louis Van Gaal alisema kuwa Van Persie hato kuwa fiti kuivaa klabu yake ya zamani ya Arsenal siku ya jumatatu katika hatua ya robo fainali ya kombe la FA.

Pia kocha huyo alisema kuwa hana uhakika kama kiungo Michael Carrick ataanza katika timu ya kwanza dhidi ya Newcastle United kwanzi ni hatari mchezaji kutoka kwenye majeruhi na kuingia kwenye timu ya kwanza moja kwa moja hivyo anafikiria kumtumia kama mchezaji wa akiba huku akisema kuwa dakika 20 za mwisho ndio anaweza kucheza.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!