.
Bunge letu la sasa linaidadi kubwa ya wabunge ambao ni vijana,wanapenda
MUZIKI na MPIRA.Cha ajabu hakuna hata mmbunge mmoja ambaye anamiliki
timu hata ya daraja la 2.Ni kweli vijana wengi hawajasoma,lakini kupitia mpira wanaweza kupata ajira.
Wabunge wengi wamekua na tabia ya kuanzisha ligi za kugombania
MBUZI,NG'OMBE,KUKU katika majimbo yao au kikombe ambacho kinathamani ya
shilingi elfu 80 na wengine huanzisha mashindano ya kugombania
JEZI.Jamani huu sio muda wa kutumia mpira ili kupata NYAMA,mpira ni
kazi.
Wabunge kutokana na nafasi yenu,mnaweza kupata wafadhili
kibao na mpira mikoani ukarudi.Badala ya kuprint tisheti na mabango
mengi wakati wa kampeni,ukiwa na timu JIMBONI kwako ambayo itakuja
kutambulika nchi nzima ni KAMPENI tosha,huna haja ya kutengeneza mabango
yakujinadi.
issue sio KILIMO KWANZA TU,mkulima aende
shamba,msanii afanye sanaa yake na mwana michezo aende kwenye
michezo.Huwezi inua michezo kwa zawadi ya MBUZI wala NGO'MBE
tu.Tunahitaji wabunge muangalie mbele zaidi.
Tuna hitaji tupate LEKA TUTIGITE nyingi kwenye soka pia.
29 August 2013
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment