NIONAVYO MIMI JUU YA KAMPENI YANGU YA KUSHAWISHI WATU WASAPOTI TIMU ZA NYUMBANI KWAO.
Hizi ndiyo sababu zangu za msingi.
1.Timu zetu nyingi za mikoani zinashindwa kuendelea kutokana na kukosa pesa,hatuna vifaa,hatuwezi kujikimu.Mashabiki ndiyo msingi wa kupata pesa ingawa kuna njia njingine pia.Unapoisapoti timu ya kwenu unachangia kukuza soka mahali unapotoka.
2.Mpira ni kazi,kwa mfano mkataba wa KELVIN YONDANI unaonyesha analipwa laki 8 kwa mwezi.Tunahitaji pia hizi pesa wazipate wadogo zetu walioko mtaani ambao wanavipaji.Watapataje? Lazima timu zetu ziwe na nguvu ya kifedha ambayo msingi wake ni mashabiki.Kitendo cha kufanya nchi nzima watu kuwa SIMBA na YANGA ni kunyima fursa wadogo zetu wa mtaani.
3.Simba na Yanga kwa sababu ya nguvu ya kifedha waliyonayo,inawafanaya wachezaji wetu kila siku wawe wanaziota hizi timu.Huwezi enda moja ya timu hizi bila kupata mtu wa kukushika mkono hata kama unakipaji kama ZIDANE.Kurudi nyuma na kusapoti timu zetu za mikoani,ni kusaidia wadogo zetu wenyewe.
4.kIUCHUMI kwa mfano wachezaji wote wa RINHO RANGERS wanakuwa wanalipwa zaidi ya milion 2 kila mwisho wa mwezi,ile pesa itazunguka pale pale TABORA na kuna uwezekano hata mama yangu muuza maandazi akanufaika na pesa hiyo.Kwahiyo badala ya kuongeza mzunguko wa pesa DAR tu,tujiongezee uwezo mikoani kwa kusapoti timu zetu.
5.Timu za SIMBA na YANGA zinauwezo wakujiongoza hata bila mchango wako wewe mtu wa MTWARA,wanawadhani na wafadhili wa kutosha.kwa nini unaendelea kumwaga maji baharini? Hapo ulipo unamdogo wako anakipaji na huna pa kumpeleka,sasa kwa nini tusiongeze fursa mikoani?? huu sio muda wa kumwaga machozi YANGA inapofungwa wakati kwenu ni MPANDA!!
6.Tuna hitaji siku moja VPL iwe na timu shiriki 20,sasa tutafikiaje hiyo idadi kama nchi nzima tuko SIMBA na YANGA? Vijana wengi wanaishi maisha ya kifahari kupitia BONGO FLAVA trust me,mpira unaweza kuajili vijana wengi kuliko muziki.Tuna weza kubadili maisha ya wadogo zetu kupitia soka,turudi kuzisaidia timu zetu za mikoani.
0 comments:
Post a Comment