Home
»
Unlabelled
» NIONAVYO MIMI KWA TAIFA STARS LEO
Leo timu yetu ya Taifa TAIFA STARS itajitupa dimbani kumenyana na ndugu
zake Emmanuel Okwi huko Uganda.Mchezo huu ni wamarudiano baada ya mechi
ya kwanza kumalizika kwa timu ya Taifa kupoteza kwa 1-0.
Kim
Poulsen kocha mkuu amewahakikishia watanzania kwamba timu inakwenda
kupata ushindi na kusonga mbele kwenye fainal za CHAN,kimpira kila kila
kitu kinawezekana ila katika uhalisia tuna kazi sana kupata ushindi
mbele ya Uganda. Vijana wetu
wanatakiwa kuwa na nidhamu ya mchezo na wakijifanya wanataka goli la
mapema bila mipango madhubuti,itakuwa kwetu.Uganda ni wazuri kuliko sisi
lakini ubora na uimara wao sio sababu ya sisi kuonekana wanyonge kila
siku.
Naamini sababu za mwezi mtukufu eti ndiyo unachangia sisi
tufungwe, leo hazitokuwepo.Mwezi wa Ramadhani unatokea mara moja tu kwa
mwaka kwahiyo isiwe sababu ya kujitetea.Ni kweli mchezaji asipokula
anapungua nguvu lakini mwezi wa Ramadhani umejikita zaidi kwenye ibada
na kwenye ibada MUNGU yupo sasa kwanini tusifuzu?
Dua zetu leo
zipo kwa STARS na inshallah Mungu atatuongoza vema,STARS inanafasi ya
kushinda na kusonga mbele.Tunajifunza kupitia makosa TBC onyesheni mechi
ili ikitokea tumefungwa benchi la ufundi na wachezaji
wasitudangaye,tujue tulipokosea na tujifunze kujipanga upya.
0 comments:
Post a Comment