Searching...
Image and video hosting by TinyPic
29 July 2013
Monday, July 29, 2013

NIONAVYO MIMI KWA JOHN BOCCO



Unapozungumzia washambuliaji wa vodacom premier league wazawa,siku zote John Bocco ndo striker wangu bora.Ukiniwekea Jerryson Tegete na Bahanuzi,bado kura yangu itakwenda kwa John Bocco.

John Bocco anavitu vingi ambavyo striker anatakiwa kuwa navyo,ananguvu,kaenda hewani,anajua kumiliki mpira na kupasia mpira wavuni.Bocco aliyezaliwa mwaka 1989 akitengenezwa vizuri na kupewa nafasi bila kumzomea,anaweza kuisaidia STARS.

Wengi wanataka kuona kila mpira anaopewa afunge goli,kitu ambacho kwenye mpira hakiwezekani.Anarekodi ya kufunga magoli mengi kwenye VPL na mfungaji bora wa muda wote wa AZAM FC.

Timu zenu hizo za simba na yanga kila siku anazitia vitasa lakini bado wengi hawamuheshimu.Bocco anajua sema tu nae anamatatizo madogo madogo kama ilivyo kwa wachezaji wengine.

Kwa sasa nadhani JOHN BOCCO anawekwa benchi na Samatta tu,Thomas ulimwengu nimemuona akiwa na kiwango cha juu kwenye mechi mbili tu za mwisho kwa hiyo,bado nahitaji kumuona zaidi ili nishawishike.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!