Searching...
Image and video hosting by TinyPic
27 July 2013
Saturday, July 27, 2013

KOCHA MKUU WA YANGA ATUA UJERUMANI


Kocha mkuu wa timu ya Young Africans mholanzi Ernie Brandts ameondoka jana usiku jijini Dar es salaam kuelekea nchini ujerumani ambapo atahudhuria kozi ya mafunzo na kuongeza muda leseni ya shirikisho la soka barani ulaya (UEFA) kwa ngazi ya daraja la kwanza.

Mafunzo ya kozi hiyo na kuongeza muda wa leseni yatafanyika kwa siku tatu (3) kuanzia siku ya jumatatu julai 29 mpaka jumatano julai 31 ambapo siku ya agosti 2 kocha anatarajiwa kurejea jijini Dar es salaam kuendelea na maandilizi ya msimu mpya wa Ligi Kuu ya Vodacom.

Brandts amekwenda kuhudhuria kozi hiyo ambayo hutolewa na shirikisho la soka barani Ulaya (UEFA) kila baada ya miaka miwili kwa makocha wenye leseni za shirikisho hilo kwa ajili ya kuongeza muda leseni hizo.

Uongozi wa klabu ya Yanga umempa baraka zote kocha Brandts kwenda kwenye kozi hiyo ambapo unaamini atakaporejea atarudi na ujuzi mwigi atakoutumia kuijenga timu na kuwa tishio katika msimu mpya wa Ligi Kuu ya Vodacom na mashindano ya kimataifa. 

Kabla ya kujiunga na timu ya Young Africans Brandts alikua akiifundisha timu ya APR kutoka nchini Rwanda ambayo alijiunga nayo akitokea kufundisha timu ya Rah Ahan ya Iran, Nac Breda, PSV Eindhoven (assistant), RKSV Nuenen, Volendam zote za Uholanzi.

Brandts ambaye alijiunga mwaka jana na watoto jangwani amaekua na mafanikio katika kikosi kwani rekodi yake katika michezo aliyoingoza Yanga imeweza kushinda michezo 16, kufungwa mchezo mmoja na kutoka sare michezo mitano (5) katika Ligi Kuu ya Vodacom.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!