Searching...
Image and video hosting by TinyPic
31 July 2013
Wednesday, July 31, 2013

NIONAVYO MIMI KWA KIM POULSEN


Mashabiki wa mpira siku zote wanataka timu yao ishinde na mambo yanapokuwa magumu,ndipo watakapoanza kupaza sauti za kuikosoa timu hata mahali pasipostahili kukosolewa.

Athumani Idd CHUJI ni kiungo mwenye uwezo mkubwa na uzoefu pia na namshukuru Kim Poulsen kwa kumpanga mechi yetu dhidi ya Uganda.Alicheza vizuri sana ila baada ya dk 90,Uganda 3,sisi 1.Asingempanga hiyo mechi zigo lote la lawama,lingekuwa mabegani mwa Poulsen.

Bado watu wanapiga kelele juu ya uwezo wa Juma Kasseja pindi anapofanya makosa ya kimchezo lakini huwezi msikia mtu akimsifia pale anapofanya "good save" kama ule mpira aliookoa kipindi cha kwanza DHIDI YA UGANDA na kuwa kona.Anyway,kuna siku JUMA KASSEJA atawekwa benchi ili roho zenu zifurahi!!

Roberto Mancini akiwa na manchester city,kila siku alikuwa anakosolewa kwa sababu ya kubadili mara kwa mara kikosi chake cha kwanza.Kim Poulsen amekuwa na kikosi chake maalumu kinachoanza lakini hili nalo limekuwa ni tatizo kwa mashabiki,mnasema eti "AMEKARIRI"

HIVI unadhani kwamba Nyoni akiwekwa benchi,Chuji akianza mechi zote na KASSEJA akienda benchi na Bathezi akaanza mechi zote ndo tutashinda?? Unadhani Bocco akienda benchi na Tegete kurudi Starz ndo itasaidia?? Kwani mara ngapi Tegete kacheza Starz? Kuna mtu aliyependwa na Maximo zaidi yake???

Tunafungwa kwa sababu ya matatizo ya kiujumla na sio mtu mmoja mmoja.Serikali,Tff,vilabu,media,wachezaji mpaka mashabiki ni sehemu ya sisi kufungwa.HATA KAMA SERIKALI ITATOA MABILION YA PESA,KAMA HAO WADAU WENGINE HAWATATIMIZA WAJIBU WAO,TUTATIWA VITASA KILA SIKU.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!