NIONAVYO MIMI ALICHOKIFANYA WENGER NDICHO ATAKACHOKIFANYA MOYES.
Chelsea wameamua kukaza uzi wa kumwitaji mshambuliaji ROONEY toka united na kwanamna mambo yanavyokwenda,Rooney anaweza kutua darajani.
Arsene wenger msimu uliopita alikuwa anakanusha kumuuza RVP kama wanavyofanya united sasa lakini muda ulipowadia RVP alitua Old Trafford,naona uwezekano mkubwa upo Rooney kwenda nje ya Old Trafford.
Arsenal baada ya mumuuza RVP na kukutananaye akiwa na uzi wa Mashetani wekundu huku akiwa amevaa sura ya kikazi,aliwafunga mechi zote na hiki ndicho watakachokipata mashabiki wa united kama Rooney atauzwa ama chelsea au timu yoyote ya EPL.
Mimi sio mtabiri naangalia ubora wa mchezaji.WAZZA ni bonge moja la striker ni aina pia ya watu ambao MOURINHO anawahitaji.Kama atakwenda kutumia pasi za mwisho toka kwa ama MATA au HAZARD,kuna siku ataondoka na mpira baada ya dk 90 dhidi ya man united iwe Old Trafford au Stanfford Bridge.
Mashabiki wa united wamepumbazwa na ubora wa RVP lakini WAZZA bado ni mshambuliaji hatari,natamani kumuona nje ya Old Trafford ili mashabiki wanaombeza wampe heshima yake.
0 comments:
Post a Comment