NIONAVYO MIMI HAYA NI MAWAZO YA KAWAIDA TU.
Kelvin Yondani aliposaini mkataba na Yanga akitokea simba alipewa mshahara wa laki 8.Mrisho Ngassa alipotoka Azam kwenda simba,mshahara wake ulikuwa millioni 2.
Kuna watumishi wengi sana wenye elimu ya chuo kikuu hawawafikii hawa jamaa kwenye mshahara na posho.Ngassa na Yondani ninauhakika wamefika hapo walipo ni kwa bidii zao binafsi na sio miundombinu madhubuti ya soka la kisasa.
Soka ni eneo pana sana ambalo maisha ya vijana wa kitanzania yanaweza kubadilika,vijana wengi sana wanaweza pata ajira na kuongeza mzunguko pesa katika jamii yetu.
Natamani kuona siku moja,viwanja vya mpira,makocha,wadhamini na wadau mbalimbali wa soka wakienea kila mtaa kama vibanda vya M-Pesa
0 comments:
Post a Comment