NIONAVYO MIMI KILA KITU KINA MMILIKI WAKE.
Hispania kupitia watoto wa La Massia wameweza kuisumbua Dunia kwa muda kama wa miaka minne sasa,wakiigeuza Dunia mwelekeo na kuwafanya watu wasahau Brazil kwa muda.Brazil ndo baba wa SAMBA style na wengine wanajaribu tu.
Naiona Hispania ambayo misingi yake imejengwa zaidi Lamasia ikianza taratibu kurudia zama zake ambazo walikuwa wanacheza mpira mzuri lakini sio wa mafanikio.Kama unakumbuka 2002,Hispania iliweza kutolewa na Korea kusini kwenye robo fainal ya kombe la dunia.
Colombia kwa sasa wamefika mpaka nafasi ya 3 kwa ubora Duniani lakini hakuna anayewatilia shaka,siku wakimfunga spain ndo wengi watashtuka.Brazil nawaona wakirudi kuchukuwa nafasi yao ambayo kwa muda sasa ilikuwa imeshikwa na spain.
ukiangalia kizazi cha xaiv,Iniesta,Cassilas,Alonso n.k na ukiangalia kizazi cha Lucas Moura,Neymar,Oscar n.k utagundua kwamba BRAZIL wamerudi upya.Spain inawatoto wengi kama kina Alcantara tatizo ni kwamba hawana nafasi timu ya Taifa.
Spain watabakia kucheza mpira mzuri lakini sio wa mafanikio tena.Wajerumani wanavijana wengi ambao wanatumika na ni hatari zaidi kama marco Reus,Gotze,Muller.VICEVT DELBOSQUE ameendelea kukariri kikosi badala ya kuanza upya kwa kuwapa vijana nafasi,hii itakula kwake.
0 comments:
Post a Comment