Imeandikwa na Dausoni Kalinjuna
MONACO SASA WAITISHA DUNIA...BAADA YA KUMNASA FALCAO, SASA WAVAMIA DARAJANI KUMCHOMOA ALIYEWAPA CHELSEA TAJI LA EUROPA LEAGUE
BEKI Branislav Ivanovic anatakiwa na Monaco baada ya kumkosa Vincent Kompany kutoka Manchester City.
Mlinzi huyo mwenye umri wa miaka 29 wa Chelsea amependekezwa na kocha Claudio Ranieri kwa mmiliki bilionea wa Kirusi, Dmitry Rybolovlev katika mpango wa kuijenga timu hiyo iliyopanda Ligi Kuu Ufaransa iwe tishio.

Walitoa oda ya Pauni Milioni 51.3 iliyokubaliwa na Atletico Madrid kwa mshambuliaji Radamel Falcao, ambaye anatarajiwa kufanyiwa vipimo leo, baada ya Ijumaa kukamilisha mpango wa kuwasajili kwa Pauni Milioni 60 wachezaji wawili wa Porto, Joao Moutinho na James Rodriguez.
Monaco ipo tayari kutoa kiasi cha Pauni Milioni 25 kumnasa Ivanovic, ambaye alifunga bao la ushindi katika fainali ya Europa League, lakini pia anatakiwa na kocha mpya wa Chelsea, Jose Mourinho.
'Special One'
alijaribu kumsajili Ivanovic msimu uliopita akiwa bado Real Madrid
lakini akakwama baada ya Chelsea kupandisha bei yake, na atataka Mserbia
huyo aendelee kuwa sehemu ya kikosi cha msimu ujao.
Pamoja na hayo atapenda kumsajili Raphael Varane wa Real Madrid na beki ambaye Mourinho anaweza kumuacha ni David Luiz, ambaye anatakiwa na Barcelona.
Monaco pia inamtaka Hatem Ben Arfa wa Newcastle.
0 comments:
Post a Comment