nadhani mashabiki wangezuiliwa kuingia na sarafu uwanjani.
mwaka 2008 Didier Drogba akiichezea chelsea vs Burnley alifunga goli na alipoenda kushangilia,alipigwa kwa sarafu.akapata hasira alipoiokota akawatupia mashabiki.alipewa adhabu kwa kitendo hiki na FA.
Rio ferdinand msimu huu alipasuliwa juu ya jicho na shabiki wa man city kwa sarafu baada ya RVP kuwapa united bao la ushindi.baadae man c wakaomba msamaha kwa tendo hilo.
Chelsea msimu huu wakati Lampard akifunga goli lake la 200 vs Westham,mashabiki walimtupia sana sarafu.kwa bahati tu hakuumia.
Swansea na Caddiff city ni simba vs Yanga pale wales na mwaka ujao wote watakuwa EPL.mwaka 2008 refa Mike Dean alipigwa na kupasuka kichwa kwa sarafu toka kwa mashabiki wa caddiff city.
nadhani wangeruhusu noti tu,sarafu zikabaki nyumbani.
0 comments:
Post a Comment