BY,JOACHIM SOLOGO
Hizi ni timu mbili ambazo miaka ya hivi karibuni zimekuwa na
desturi ya kuuza wachezaji wake wengi pengine kwa sababu ya kujenga uchumi wa
timu husika. Kwa mfano miaka ya hivi karibuni tumeshuhudia Arsenal ikiwauza
nyota wake muhimu kama vile Samir Nasri, Gael Clichy, Cesc Fabrigas, Alex Song,
Robin Van Persie achilia mbali wengineo kama vile Mathiew Flamin, Thiery Henry
na Vieira.
Kwa upande wake Porto
imewauza wachezaji kama vile Deco, Hulk, Radamel Falcao, Deco De Souza, Maicon,
Bosingwa, Pepe, Anderson, Quaresma, Raul Meireles na wengine wengi. Lakini pia FC PORTO wamewauza makocha wao
kama vile Jose Mournho na Andre Via Boaz. Kwangu mimi naona Arsenal na Porto
wamefanana katika sela ya kuuza nyota wao bila kujali umuhimu wao katika timu,
lakini FC PORTO wamewazidi Arsenal katika kipengele kimoja muhimu sana. Hiki ni
kipengele cha mafanikio.
Pamoja na kwamba FC Porto wanauza sana wachezaji wao lakini
bado wamekuwa wakichukua makombe kama kawaida. Kwa Arsenal hali ni tofauti
maana wamekuwa na misimu mingi bila kuchukua kombe lolote. Wanauza wachezaji na
hawapati makombe, labda kama kombe la Emirates nalo linaingizwa kwenye record.
Swali la kujiuliza ni hili; ni wapi Arsenal wanapokosea? Je falsafa yao wameshindwa
kuitumia? Kumbuka kwamba FC PORTO wanarekodi ya kutwaa makombe yote muhimu kama
vile UEFA CHAMPIONS LEAGUE NA UEFA EUROPA CUP na hata yale ya nchini kwao
Ureno.
“I SALUTE YOU FC
PORTO” VIVA FC PORTO!!!!!
0 comments:
Post a Comment