Searching...
Image and video hosting by TinyPic
22 May 2013
Wednesday, May 22, 2013

simba na yanga wanatakiwa kubadilika.

                                                    

simba na yanga wanatakiwa kubadili mtazamo na kuamini kuwa,wanamashabiki wengi mikoani kuliko DAR hivyo,badala ya pre-season kwenda Uturuki na Oman waje milayani hasa kule ambako hakuna timu inayoshiriki ligi kuu.

Simba na yanga wakipita kila wilaya wataibua mashabiki kibao na watauza vifaa vyao kibao.nadhani wanatakiwa kuwapa nafasi mashabiki ambao huwa hawapati fursa ya kuwaona Dar.

Zamani wakati nimeanza kucheza mpira nilikuwa nikijiita "captain Dunga ingawa hata danadana sikuwa naweza" najua na wewe ulijiita majina hayo ya majuu kwa sababu nilikuwa naona mpira kwenye TV wa Ulaya na watanzania nilikuwa nauskia tu Radion ukitangazwa.

Simba na yanga wakitembelea kila wilaya baada ya mwezi,kuna watoto wengi watajiita NGASSA,KASSEJA,YONDANI,CHUJI,KAZIMOTO na kuandika nyuma ya mashati yao wakiwa ligi za mchangani.

Njooni wilayani bwana,watu hatuna pa kufikia huko DAR

                                           

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!