Searching...
Image and video hosting by TinyPic
24 January 2015
Saturday, January 24, 2015

Mchezaji aliyembioni kukimbia kwenye kikosi cha Mourinho.


Na Chikoti Cico

Winga wa klabu ya Chelsea Andre Schurrle anaweza kuuzwa na klabu hiyo kutoka jijini London kwenye dirisha hili dogo la usajili kwa mwezi Januari kama ikitokea ofa nzuri kutoka klabu mbalimbali zinazomhitaji mchezaji huyo.
Kocha wa Chelsea Jose Mourinho ambaye amedai hatauza wala kununua mchezaji yeyote kwenye dirisha hili dogo la usajili hakuonyesha kupinga taarifa za Schurrle kuweza kuondoka kwenye klabu hiyo wakati akiongea na waandishi wa habari siku ya Ijumaa kuelekea mchezo wa kombe la FA dhidi ya Bradford.
Akiongea na waandishi wa habari kuhusu kuondoka kwa Schurrle alisema “msimamo ni kwamba tungemhitaji (Schurrle) kubaki, swali sio kama anaruhusiwa kundoka ama hapana. Swali sio kama tutapata ofa nzuri, swali ni kama tuna ofa kubwa sana na mchezaji kupenda sana kukubaliana na changamoto mpya kwenye kazi yake kwasababu hatuhitaji kuuza wachezaji wetu”.
Mchezaji huyo kutoka Ujerumani ambaye alisajiliwa Chelsea kutoka klabu ya Bayer Leverkusen amekuwa hana namba ya kudumu kwenye kikosi cha kwanza cha kocha wa Chelsea Jose Mourinho na taarifa kutoka vyombo mbalimbali vya habari zinasema klabu ya Vfl Wolfsurb tayari imetuma ofa kwa klabu ya Chelse kutaka kumsajili mchezaji huyo.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!