Searching...
Image and video hosting by TinyPic
24 January 2015
Saturday, January 24, 2015

Asamoah Gyan aibeba Ghana AFCON.


Na Chikoti Cico

Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Ghana Asamoah Gyan ambaye alikuwa akisumbuliwa na Malaria mwanzoni mwa michuano ya kombe la Mataifa ya Afrika alirejea uwanjani jana kwenye mchezo dhidi ya Algeria na kuipatia ushindi timu ya Ghana maarufu kama Black Stars.
Katika mchezo huo ambao ulikuwa na nafasi chache za magoli iliwachukua Ghana mpaka dakika ya 92 ya mchezo kupata goli la ushindi baada ya Gyan kuukokota mpira mrefu uliopigwa na Mubarak Wakaso kabla ya kuachia shuti kali la mguu wa kulia na mpira kujaa wavuni.
Kutokana na ushindi huo Ghana wanashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa kundi C nyuma ya Senegal ambao wanaongoza kundi hilo wakiwa na alama nne, alama tatu walizopata dhidi ya Algeria zimefufua matumaini ya Ghana kuvuka hatua ya makundi baada ya kupoteza mchezo wa kwanza dhidi ya Sengal.
Mchezo mwingine wa kundi C maarufu kama “kundi la kifo” ulikuwa ni mchezo kati ya Senegal dhidi ya Afrika ya Kusini uliochezwa kwenye uwanja wa Estadio de Mongomo, mpaka mwisho wa mchezo huo matokeo yalikuwa ni sare ya goli 1-1
Afrika ya Kusini maarufu kama Bafana Bafana ndiyo walikuwa wa kwanza kupata goli kupitia kwa Oupa Manyisa kwenye dakika ya 47 ya mchezo kabla ya S. Kara Mbodji kuisawazishia Senegal kwenye dakika ya 60 na mpaka mwisho wa mchezo huo matokeo yalibaki kuwa 1-1.
Kutokana na matokeo hayo Senegal ambao wanaongoza kundi C watahitaji alama moja tu kwenye mchezo wa mwisho dhidi ya Algeria ili kuvuka hatua ya makundi huku Afrika ya Kusini ikiombea Senegal waifunge Algeria na wao waifunge Ghana ili kuweza kuvuka pia hatua ya makundi.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!