Searching...
Image and video hosting by TinyPic
4 December 2014
Thursday, December 04, 2014

Bayern Munich wamejiondoa rasmi.


 Na Oscar Oscar Jr

Mabingwa wa Bundesliga, timu ya Bayern Munich wameamua kujiweka pembeni kwenye mbio za kumnasa kiungo mshambuliaji wa Borussia Dortmund, Marco Reus. 

Kujiondoa huko kwa miamba hao wa Ujerumani kunafungua milango kwa timu za Manchester United na Liverpool ambao wamekuwa wakitajwa kumuwania mchezaji huyo.

Kupitia kwa mkurugenzi wa michezo wa Bayern Munich, Matthias Sammer leo hii amekanusha habari ambazo zilikuwa zimeenea kuwa tayari Pep Gaurdiola amemsana winga huyo. 

Matthias amesema kuwa hakuna habari kama hizo na hakuna mawasiliano yoyote yanayomuhusu mchezaji huyo kutua Allianz Arena.

Bayern Munich kwa miaka miwili ya hivi karibuni, wamefanikiwa kuwadhoofisha mahasimu wao Borussia Dortmund kwa kuwachukuwa kiungo mshambuliaji, Mario Gotze na Striker, Robert Lewandowski. 

Dortmund wako vibaya kwenye ligi kuu licha ya kufuzu kwenye klabu bingwa Ulaya kwa hatua ya mtoano na matokeo hayo yanaweza kumshawishi Reus kuikacha timu hiyo.

Klabu za Uingereza zimekuwa zikitajwa kumnasa mchezaji huyo ingawa wili iliyopita kocha wa klabu ya Chelsea, Jose Mourinho alinukuliwa akisema kuwa, timu yake haina mpango na mchezaji huyo. 

Hii inaweza kuwa habari njema kwa timu za Liverpool na Manchester United ambao wanaonekana kummezea mate mchezaji huyo.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!