Searching...
Image and video hosting by TinyPic
9 December 2014
Tuesday, December 09, 2014

Uchambuzi: Liverpool vs Fc Basel




Na Chikoti Cico


Mchakamchaka wa kumalizia michezo ya hatua ya makundi kwenye ligi ya mabingwa Ulaya unatarajiwa kuendelea tena Jumanne na Jumatano ya wiki hii, huku kwenye uwanja wa Anfield Liverpool wakiikaribisha Fc Basel katika moja ya mechi za kundi B ambapo Liverpool watahitaji ushindi huku Basel wakihitaji sare ili kuvuka hatua ya makundi.
 
Liverpool ambayo inashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa kundi B ikiwa na alama nne inatarajia kuingia kwenye mchezo huo kucheza kufa na kupona ili kupata ushindi na kuingia hatua ya mtoano ili kuungana na Real Madrid ambao washavuka kutoka kundi hilo.

Wakati huo huo timu ya Liver itawakosa Daniel Sturridge na Mario Balotelli katika safu ya ushambuliaji hivyo kocha wa timu hiyo Brendan Rodgers anatarajia kumwanzisha Rick Lambert ambaye ameonyesha kiwango kizuri kwa mechi za karibuni.

Kuelekea mchezo huo takwimu zinaonyesha Liverpool wamekuwa na rekodi nzuri dhidi ya timu kutoka Uswisi kwani katika mechi 10 imeshinda mechi sita, kutoka sare mechi tatu na kufungwa mechi moja.

Kikosi cha Liverpool kinaweza kuwa hivi: Mignolet; Johnson, Skrtel, Lovren, Moreno; Henderson, Lucas, Gerrard; Lallana, Lambert, Coutinho

Upande wa timu ya Basel ambao wanahitaji  sare tu ili kuweza kuingia hatua ya mtoano watawakosa Giovanni Sio na Ivan Ivanovic ila Geoffroy Serey Die anatarajiwa kurejea kikosi baada ya kutumikia adhabu ya kuwa nje kwa mechi mbili baada ya kuonyeshwa kadi nyekundu.

Huku wakiwa na alama sita na kushika nafasi pili kwenye msimamo wa kundi B Basel sio timu ya kubeza hasa ikizingatiwa ilimfunga Liverpool goli 1-0 katika mechi ya kwanza iliyofanyika nyumbani kwa Basel nchini Uswisi.

Nao Basel wameonekana kuwa na takwimu nzuri kwa mechi za karibuni dhidi ya timu za Kiingereza kwani imeweza kushinda mechi tatu zilizopita dhidi ya timu kutoka Uingereza huku wakiifunga Chelsea mara mbili na Liverpool mara moja.

Kikosi cha Basel kinaweza kuwa hivi: Vaclik; Degen, Samuel, Schar, Xhaka; Aliji, Delgado, Calla, Ahmed; Streller, El Nenny.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!