Searching...
Image and video hosting by TinyPic
24 January 2015
Saturday, January 24, 2015

Ronaldo alimwa kadi nyekundu Madrid ikishinda

Na Chikoti Cico


Mshambuliaji wa klabu ya Real Madrid na mchezaji bora wa dunia mara tatu Christiano Ronaldo atolewa nje kwa kadi nyekundu kwenye mchezo wa ligi kuu nchini Hispania maarufu kama La Liga kati ya Cordoba dhidi ya Real Madrid.
Ronaldo ambaye hakuonekana bora kwa sehemu kubwa ya mchezo huo alionyeshwa kadi hiyo nyekundu kwenye dakika ya 82 ya mchezo baada ya kumpiga kichwani beki wa Cordoba Jose Angel Crespo.

Mchezo huo uliisha kwa Real Madrid kushinda kwa magoli 2-1 ambapo timu ya Cordoba ilikuwa ya kwanza kupata goli kwenye dakika ya tatu ya mchezo kwa njia ya penati iliyopigwa na Nabi Ghilas baada ya shuti la Bebe kuugonga mkono wa beki wa Madrid Sergio Ramos na mwamuzi aliamuru ipigwe penati.

Nayo timu ya Real Madrid ilisawazisha goli hilo kwenye dakika ya 27 ya mchezo kupitia kwa Karim Benzema aliyeunganisha mpira wa kona uliopigwa na James Rodriguez, huku mchezo ukikaribia kuisha kwenye dakika ya 89 Gareth Bale aliipatia Madrid goli la pili na la ushindi kwa njia ya penati baada ya mpira wa adhabu aliopiga kuzuiwa kwa mkono na beki wa Cordoba

Hivyo hadi mwisho wa mchezo Madrid walitoka kifua mbele kwa ushindi wa magoli 2-1, wakati huo huo kutokana na kitendo kilichopelekea Christiano Ronaldo kuonyeshwa kadi nyekundu kwenye mchezo huo inawezekana akapewa adhabu ya kufungiwa mechi tatu.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!