Searching...
Image and video hosting by TinyPic
3 December 2014
Wednesday, December 03, 2014

JUMA ABDUL ATAPOTEZWA NA MARCIO MAXIMO.


Na Samuel Samuel

  Na Samuel Samuel
 
Msimu wa 2013-14 Hamis Tambwe ndiye aliyeibuka mchezaji kinara kwa kuifungia Simba SC magoli 19. Thamani ya mchezaji huyo ilionekana kubwa na kuanza kuwakumbusha wana msimbazi mchezaji wao mahiri wa wakati huo, Nteze John " Rungu". 

Tambwe alionekana lulu na kuyafanya maisha yake ndani ya msimbazi kuwa ya thamani sana kuliko hata mkongwe Chollo ambaye kwa sasa ni mmoja wa wachezaji wakongwe walioko kwenye kikosi hicho. Wahenga wanasema " kipya kinyemi " .

Ujio wa kiungo mshambuliaji Emmanuel Okwi kutoka Dar Young African, ulizima kabisa mshumaa wa heshima wa mchezaji huyo. Nyoyo za wana msimbazi zilipambwa na mganda okwi na kumsahau shujaa wao . 

Huwa najiuliza kama Tambwe asingelifunga magoli hayo Simba ingemaliza ya 19? Ni kweli Tambwe kaisha au mfumo wa nani bora na kaletwa na nani unatumika? 

Ujio wa Okwi umekidumaza kipaji cha Tambwe, si kocha wala shabiki anaetaka kumsikia Tambwe. Mfano huo hapo juu unaweza kuwa mwiba mchungu kwa kinda mkomavu, Juma Abdul jezi namba 12 mgongoni ambaye anakipiga kikosi cha kwanza wana jangwani " Dar Young African". 

Toka kocha Brandts akiwepo, Juma Abdul ambaye anacheza beki ya kulia alionesha kujituma na kuwa mbadala sahihi wa mrundi, Mbuyu Twite ambaye kwa sasa anacheza kama kiunngo mkabaji baada ya Frank Domayo kumtimkia Azam FC mwanzoni kabisa wa msimu huu. 

Juma ana uwezo mzuri wa kupandisha timu na kucheza muda mrefu bila kuchoka. Hayo aliyathibitisha mwishoni mwa msimu wa 2013-14 baada ya Mbuyu Twite kuumia. 

Kocha Hans Van der Pluijm, alimwamini kijana na akafanya kweli na kujihakikishia namba ya kudumu ya nafasi hiyo adhimu kabisa ndani ya Yanga. Nafasi ambayo imepitiwa na wachezaji mahiri kabisa ndani ya klabu hiyo kama Ngadou Ramadhani, Fredi Mbuna na Shadrack Nsajigwa " fusso". 

Ujio wa Emerson kutoka nchini Brazil unahatarisha nafasi ya beki huyo. Unajua kwa nini? Emerson ambaye amesaini kandarasi ya mwaka mmoja ni kiungo mkabaji ambayo nafasi hiyo kwa sasa inashikiliwa na Mbuyu Twite ambaye kiasilia ni beki wa kulia. 

Hakuna asiyejua kazi ya mrundi huyo akisimama kama beki namba mbili. Piga ua Maximo itamlazimu kumrudisha Mbuyu Twite kulia kama beki namba mbili ili Emerson alimiliki dimba la kati. 

Hali hiyo itamlazimu Juma Abdul kurudi benchi. Taa ya mafanikio ilianza kung'aa na sasa inaelekea kuzimika ghafla. Makocha wengi hawapendi kufanya majaribio na nafasi ya ulinzi, kama wachezaji wa kikosi cha kwanza wakitengeneza kombinesheni nzuri basi huachwa kwa muda mrefu ili wazoeana. 

Hapo Abdul itambidi angoje Twite aumie ndo apate nafasi. Sidhani kama Maximo atakuwa na hekima ya kumweka benchi Mbuyu Twite ili apokezane na Emerson. Emerson atashikilia dimba hilo akipokezana na Omega Seme dalili zinaonesha hivyo. 

Hivyo basi nampa rai mdogo wangu Juma Abdul akae chonjo na maamuzi yoyote yale ambayo Maximo atachukua

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!