Searching...
Image and video hosting by TinyPic
24 December 2014
Wednesday, December 24, 2014

Ukisikia Mdomo uliponza kichwa, ndiyo hii.


Na Chikoti Cico

Kiungo wa Barcelona ambaye anacheza kwa mkopo timu ya West Ham Mkameruni Alex Song ameachwa kwenye orodha ya wachezaji watakaoiwakilisha timu ya taifa ya Kameruni kwenye michuano ya Mataifa ya Afrika kwa mwaka 2015 itakayofanyika nchini Equatorial Guinea.

Song ambaye alipewa kadi nyekundu kwenye mchezo dhidi ya Croatia kwenye michuano ya kombe la Dunia iliyofanyika nchini Brazili mapema mwezi Julai, tokea wakati huo amekuwa hana mahusiano mazuri na shirikisho la soka la nchini Kameruni (FECAFOOT).

Taarifa za kuachwa kwa Song kwenye kikosi hicho cha Kameruni zimepokelewa kwa furaha na kocha wa West Ham Sam Allardyce ambaye kwasasa atawakosa wachezaji wawili tu ambao ni Diafra Sakho na Cheikhou Kouyate wa Senegal wakati michuano hiyo itakapoanza hapo Januari 17, 2015.

Song ambaye aliwahi kuicheze timu ya Arsenal kabla ya kusajiliwa na Barcelona amekuwa na mchango mkubwa kwenye timu ya West Ham huku akiisaidia safu ya kiungo ya timu hiyo kung’ara na kupelekea timu hiyo kuwepo kati ya timu nne za juu (top four) kwenye msimamo wa ligi wakiwa na alama 31.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!