Searching...
Image and video hosting by TinyPic
27 June 2013
Thursday, June 27, 2013

VAN PERSIE NA CRISTIANO RONALDO VS MESSI NA NEYMAR...DUNIA ITATIKISIKA 'WALLAH'


FIKIRIA kuwachezesha Cristiano Ronaldo na Robin van Persie kwenye safu ya ushambuliaji ya timu yako dhidi ya timu ambayo Neymar na Lionel Messi wanaongoza mashambulizi yake?
 
Unapozungumzia fantasy football (Soka la ndoto)…. hili ndiyo kiboko yao.
Kampuni ya Fans All Star Football (FAS) inawapa nafasi mashabiki wa soka duniani kote kuchagua kikosi chao cha wakipendacho kutoka kwa wachezaji bora Ulaya na duniani kwa ujumla.
 
Baada ya upigaji kura kumalizika mashabiki wa soka watapata nafasi ya kushiriki shindano la kupambana na timu iliyochaguliwa na wataalamu wa soka na kushindani kiasi cha pauni milioni 50,000.
 
Superstar: Real Madrid's Portuguese forward Cristiano Ronaldo is one of the players available listed for Europe
Supa Staa: Mshambualiaji wa Real Madrid, Mreno Cristiano Ronaldo yupo kwenye orodha ya nyota wa Ulaya
Fantasy pick: Cristiano Ronaldo shows off his buff body while on holiday in Miami and (inset) cartoon character Johnny Bravo
Cristiano Ronaldo akionyesha mwili wake uliojengeka akiwa Miami (picha ndogo) katuni Johnny Bravo 
Kuepusha zoezi hilo kuwa gumu, mfumo unatumika ni 4-4-2.  Fikiria Ronaldo, Gareth Bale, Andrea Pirlo na David Beckham kwenye timu moja? Van Persie atatengenezewa nafasi kibao. Hiyo inaweza kuwatisha mabeki lakini ni bonge la burudani kwa mashabiki.
 
Tofauti na kura za Fans All Star Global, wale watakaoshiriki watapata nafasi ya kuonyesha uwezo wao kwenye soka kwa kupambana na magwiji kwenye Shindano la FAS.
 
Mashabiki watapata nafasi ya kushinda kiasi cha pauni 50,000 kama wakifanikiwa kutengeneza kikosi kama kile ambacho kitatengenezwa na wataalamu wa Fans All Star ambao ni Kocha wa zamani wa England, Glenn Hoddle na Muargentina Bingwa wa Kombe la Dunia, Ossie Ardiles. 
 
Robin van Persie
Gareth Bale
Viwango vya dunia: Robin van Persie na Gareth Bale ni miongoni mwa nyota wa Ligi Kuu England
Duo: Barcelona talisman Lionel Messi and his new team-mate Neymar lead the Rest of the World talent
Wawili: Mkali wa mabao wa Barcelona, Lionel Messi na mchezaji mwenzake mpya, Neymar wanaongoza vipaji vingine duniani
Neymar
Prize: Fans All Star allows users to pick their teams and take on a team of experts for the chance to win £50k
Zawadi: Watumiaji wa Fans All Star wanaruhusiwa kuchagua timu na kupambana na timu ya wataalamu kuwania pauni 50,000
Star studded: FAS lets football fanatics to pick their Europe and Rest of the World teams
Chagua timu yako ya FAS 
Fans All Star logo
Ilikufanikiwa katika hili mashabiki watatakiwa kununua ‘bundles’ za Kura na kuingiza vikosi vya ziada.
Washiriki wa Fans All Star wataweza kuchagua kikosi cha wachezaji 15 cha kikosi cha Ulaya na kile cha kikosi cha Ulimwengu mzima (Wachezaji 11 wa kuanza na wanne wa benchi) wachezaji hao watakuwa kati ya wachezaji bora 1100, 550 watakuwa wa Ulaya na 550 wengine watakuwa wa Ulimwengu wote.
Jumatatu ijayo idadi ya kwanza ya wachezaji 1100 itapunguzwa kufiki 660 kutokana na kura za mashabiki, idadi hii itapunguzwa tena Alhamisi ya Agosti 1 na kubaki 110, upigaji kura utafika tamati Agosti 31 mwaka huu.
 
Kikosi cha kwanza cha wataalamu wa Fans All Star kitatangazwa Jumanne ya Septemba 1 mwaka huu.
Kuchagua timu yako Ulaya na Ile ya Dunia unatakiwa kuingia kwenye mtandao wa www.fansallstar.com

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!