TIMU ya taifa ya Brazil imeshinda mechi
yake ya pili ya Kombe la Mabara, huku kijana mdogo mwenye kipaji cha
ajabu, Neymar akifunga bao tamu ndani ya dakika 10 za kwanza kabla ya
kumtengenezea nafasi ya kufunga bao la pili
Brazil imeilaza Mexico mabao 2-0 bila ubishi na sasa inatimiza ponti sita na kuzidi kujiimarisha kileleni mwa Kundi A.
Daniel Alves alipinda krosi kutoka kulia
na nyota mpya wa Barcelona, Neymar akaitokea wa kwanza mbele ya beki wa
Mexico, kabla ya kuhadaa na kumtungua kipa Jose Corona dakika ya tisa
na dakika ya 90 akampa pande Jo kufunga la pili.
Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa
Howard Webb wa Uingereza, kikosi cha Brazil kilikuwa: Cesar, Alves,
Silva, Luiz, Marcelo, Luiz Gustavo, Paulinho, Oscar/Hernanes dk62,
Hulk/Lucas Moura dk78, Neymar na Fred.
Mexico:
Corona, Rodriguez, Salcido, Torrado, Dos Santos, Henandez, Moreno,
Guardado, Torres/Barrera dk70, Mier na Flores/Herrera dk68.
Balaa: Neymar alikuwa shujaa wa Brazil leo
Pongezi: Neymar akishangilia bao lake
Javier Hernandez akiwa chini baada ya kukutana na shuluba la Thiago Silva
Damu! David Luiz aliumizwa kichwani na beki mwenzake wa kati, Thiago Silva hadi kutokwa damu
Luiz akitibiwa
Damu ilisababisha abadilishe jezi
Mbio: Neymar akijaribu kumtoka Gerardo Torrado wa Mexico
Hulkl akipambana na Jorge Torres Nilo wa Mexico
Shabiki wa Brazil
Neymar akiugulia maumivu katika moja ya matukio ya mechi hiyo baada ya kuumia
0 comments:
Post a Comment