Searching...
Image and video hosting by TinyPic
21 January 2015
Wednesday, January 21, 2015

Hakuna mbabe Liverpool vs Chelsea


Na Chikoti Cico

Mchezo wa fainali ya kwanza ya kombe la Capital One kati ya Liverpool dhidi ya Chelsea uliochezwa kwenye uwanja wa Anfield usiku wa Jumanne ulimalizika kwa matokeo ya sare ya goli 1-1.

Chelsea walikuwa wa kwanza kupata goli kwenye dakika ya 18 kwa njia ya penati iliyopigwa na Edez Hazard baada ya kuangushwa na Emre Can kwenye eneo la hatari, goli hilo liliwafanya Liverpool waje juu kutaka kusawazisha lakini mpaka timu zinaenda mapumziko Chelsea walitoka kifua mbele kwa goli hilo moja.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi huku Liverpool wakitawala sehemu kubwa ya kipindi hicho kwa pasi za haraka na kulishambulia lango la Chelsea mara kwa mara na kwenye dakika ya 59 alikuwa ni Reheem Sterling aliyeipatia Liverpool goli la kusawazisha baada ya kukimbia na mpira kwa yadi 26 kuelekea langoni mwa Chelsea kabla ya kuachia shuti kali kwa mguu wa kushoto na mpira kujaa wavuni.

Baada ya goli hilo Liverpool waliendelea kuliandama lango la Chelsea na kama sio uimara wa kipa Thibaus Courtios basi vijana wa Brendan Rodgers wangeweza kuondoka na ushindi kwenye mchezo huo uliokuwa mkali na wa kusisimua.

Hivyo mpaka mwamuzi wa mchezo huo Martin Atkinson anapuliza kipyenga kuashiria kumaliza mchezo huo matokeo yalibaki kuwa sare ya goli 1-1 na hivyo macho na masikio ya wapenzi wa timu hizo mbili yatakuwa ni kwenye mchezo wa marejeano utakaofanyika wiki ijayo kwenye uwanja wa Stamford Bridge.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!