Searching...
Image and video hosting by TinyPic
21 January 2015
Wednesday, January 21, 2015

Ivory Coast washikwa na Guinea


Na Chikoti Cico

Mchezo wa kundi D kati ya Ivory Coast dhidi ya Guinea uliochezwa kwenye uwanja wa Estadio de Malabo nchini Guinea Ikweta katika mfululizo wa mechi za kombe la Mataifa ya Afrika uliisha kwa sare ya goli 1-1.

Katika mchezo huo Guinea walikuwa wa kwanza kupata goli kwenye dakika ya 36 kupitia kwa Mohammed Yattara baada ya kuachia shuti kali lililokwenda moja kwa moja wavuni baada ya mabeki wa Ivory Coast kushindwa kuondosha mpira kwenye eneo la hatari.

Pamoja na Ivory Coast kulishambulia lango la Guinea wenye kipindi cha kwanza lakini mpaka timu zinaenda mapumziko walikuwa Guinea waliotoka kifua mbele kwa goli hilo moja baada ya kuonyesha nidhamu kubwa ya kulilinda lango lao.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi huku Ivory Coast wakitafuta goli la kusawazisha na Guinea wakilinda goli lao moja, kwenye dakika ya 58 Gervinho ambaye alionyesha mchezo mzuri alipewa kadi nyekundu baada ya kumpiga mchezaji wa Ivory Coast kichwani na hivyo kuipa kazi ngumu safu ya ushambuliaji ya Tembo hao kusawazisha goli hilo.

Huku mchezo ukizidi kushika kasi na Ivory Coast wakizidi kulishambulia lango la Guinea kwenye dakika ya 72 Seydou Doumbia aliipatia Ivory Coast goli la kusawazisha baada ya kupokea pasi kutoka kwa Wilfried Bony.

Hivyo mpaka mwisho wa mchezo matokeo yalibaki kuwa sare ya goli 1-1 huku wachezaji mahiri wa Ivory Coast Yaya Toure, Wilifried Bony, Cheick Tiote wakibaki wameduwaa bila kutegemea matokeo hayo.

Vikosi vya timu zote mbili vilikuwa hivi: Guinea: N. Yattara, Is Sylla, Pogba, F Camara, Sankoh, Kéita, Fofana, Constant, Conté, Traoré, M. Yattara (Abdoul Camara 67’)

Ivory Coast: Gbohouo, Aurier, K. Touré, Bailly, Kanon, Serey Dié (Tiene 64’), Tioté, Y. Touré (Doukoure 86’), Kalou (Doumbia 64’), Bony, Gervinho

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!