Searching...
Image and video hosting by TinyPic
21 January 2015
Wednesday, January 21, 2015

Romario aangukia penzi la dogodogo


Na Chikoti Cico

Mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Brazili Romario de Souza ameangukia kwenye penzi la binti mdogo mwenye umri wa miaka 19 aitwaye Dixie Pratt ambaye ni mwanamuziki.

Romario mwenye umri wa miaka 48 ambaye amempita binti huyo karibu miaka 30 ameonekana kupata mpenzi huyo mpya baada ya binti huyo kubandika picha mbalimbali kwenye mtandao wa instagram zikiwaonyesha yeye na Romario wakiwa mapumzikoni kwenye kisiwa cha Karibian cha Aruba.

Inaeleweka kwamba Romario alimpata binti huyo mwaka 2013 baada ya kuachana na mke wake Isabella Bittencourt.

Tofauti ya umri wa umri wa miaka 29 kati ya Romario na binti huyo inamaanisha mpenzi wake huyo mpya hakuwa amezaliwa wakati mshambuliaji huyo wa zamani wa Brazili anafunga magoli matano na kuisaidia Brazili kuchukua kombe la Dunia mwaka 1994 Atlanta Marekani.

Romario ambaye alichaguliwa kama mchezaji bora wa Dunia mwaka huo huo wa kombe la Dunia amefunga jumla ya magoli 55 katika michezo 70 aliyoichezea timu ya taifa ya Brazili maarufu kama Selecao.

Pia mshambuliaji huyo aliwahi kuzichezea klabu za PSV Eindhoven na Barcelona zakutoka barani Ulaya kabla ya kurejea nchini Brazili kuichezea klabu ya Vasco Da Gama ambapo ndipo alipomalizia soka lake kabla ya kustaafu.

Na tangu baada ya kustaafu soka Romario amekuwa akijihusisha na mambo ya siasa huku akikiwakilisha chama cha “Socialist Party” na alikuwa mmoja ya watu walioshutumu kufanyika kwa kombe la dunia nchini Brazili kwa mwaka 2014.


0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!