Searching...
Image and video hosting by TinyPic
1 February 2015
Sunday, February 01, 2015

Chelsea vs Manchester City hakuna mbabe.


Na Chikoti Cico
.
Ligi kuu nchini Uingereza iliendelea tena wikendi huu ambapo nyasi za viwanja mbalimbali viliwaka moto ambapo kwenye uwanja wa Stamford Bridge timu ya Chelsea ilikuwa ikipepetana na Manchester City mchezo ambao ulivuta hisia za mashabiki wengi wa soka duniani.
Tofauti na matarajio ya wengi mchezo huu ulionekana kupoa kwa sehemu kubwa ya kipindi cha kwanza huku kila timu ikijaribu kulinda lango lake zaidi kuliko kushambulia na kwa sehemu kubwa eneo la kati kati ya uwanja lilidhibitiwa zaidi na viungo wa timu zote mbili.
Iliwachukua Chelsea mpaka dakika ya 41 ya kipindi cha kwanza kupata goli kupitia kwa Loic Remy aliyeunganisha krosi safi ya Eden Hazard goli lililoamsha kelele za mshabiki waliokuwa wamejazana kwenye uwanja wa Stamford Bridge, dakika nne 4 baadaye Manchester City walifanikiwa kusawazisha goli hilo kupitia kwa David Silva akiunganisha shuti kali la Sergio Aguero lililokuwa linaelekea nje hivyo mpaka timu zote zikienda mapumziko matokeo yalikuwa ni 1-1.
Kipindi cha pili kilianza kwa City kuonekana kutafuta goli zaidi na kasi ya mchezo ilionekana kuongezeka, ni katika kipindi cha pili ndipo vijana hao wa Manuel Pellegrini walionekana kulishambulia sana lango la Chelsea lakini juhudi za Aguero, Navas na Milner hazikuzaa matunda kubadilisha matokeo hayo.
Chelsa walioingia kwenye mchezo huo bila ya mshambuliaji wake hatari Diego Costa na kiungo Cesc Fabregas kwa sehemu kubwa ya kipindi cha pili walionekana kulinda zaidi kutokufungwa kuliko kushinda na mpaka mwamuzi wa mchezo huo Mark Clattenburg anapuliza kipyenga kumaliza mchezo huo matokeo yalibaki kuwa goli 1-1. Hivyo Chelsea kufikisha alama 53 na Man City alama 48.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!