Searching...
Image and video hosting by TinyPic
3 December 2014
Wednesday, December 03, 2014

Kwa nini Mrisho Ngassa hajang'aa mpaka sasa?


Na Samuel Samuel 
0652464525

Hans Pluijm, mchawi wa samba Jangwani anakumbukwa zaidi na wanazi wa timu hiyo kutokana na mifumo yake ya kushambulia. Ni kocha ambaye hajawahi kubeba kombe lolote na timu hiyo wala kuifunga Simba SC kama ilivyo ada kwa vilabu vyetu hivi viwili lakini aliagwa kwa sherehe. 

Pluijm aliiwezesha klabu hiyo kushika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi hali iliyoifanya klabu hiyo kulitema kombe. Mbali na hayo yote lakini wana Yanga huwaambii kitu kwa mzee huyo aliyeitumikia Yanga miezi sita tu. 

Unajua kwa nini anahusudiwa zaidi huyu babu ? Hans aliifanya yanga kuogopwa kutokana na mfumo wake wa kushambulia na kujilinda. Timu iliimarika zaidi eneo la kiungo cha kati alipokuwa anasimama kijana Domayo na safu nzima ya ushambuliaji. 

Hans ndiye aliyemfanya Ngasa aibuke mfungaji bora wa klabu bingwa Afrika kwa kutupia magoli sita dhidi ya Wacomoro. Mbali na hilo, kiungo huyo mshambuliaji alimaliza ligi akiwa na magoli 13 lakini kwa sasa hana goli hata la off side licha ya kucheza mechi zote saba. 

Hans aliitengeneza Yanga ikawa na uwezo wa kushambulia kupitia idara zote. Mbali na majukumu ya ulinzi aliwaruhusu mabeki wa pembeni kupandisha timu na hivyo kuifanya timu kuwa na kasi ya ajabu. 

Wakati beki zinapanda aidha ndani ya 4-4-2 au 4-5-1, basi viungo wote pamoja na mshambuliaji wa kati wanasogea mbele kutengeneza striking base. 

Hapo tisa " Kavumbagu " au Ngassa walikuwa na uwezo mkubwa wa kupokea mipira mizuri toka pembeni na kutokana na striking base ya viwango wakabaji basi timu si rahisi kupoteza mpira . ndo maana watu walikuwa wanapigwa saba. 

Ngasa anahitaji eneo kubwa ili atengeneze kasi ya kufunga. Kiasilia si " one - two player" . Maximo anashambulia kupitia kati na hataki mchezaji yoyote yule akae na mpira. Hali hiyo inamfanya Twite kuachia mpira haraka , Niyonzima kutosogea juu kwa kasi na kuachia mpira kabla hata beki line ya timu pinzani haijapanda juu. 

Hapo Ngassa au tisa mshambuliaji hupokea mpira kati kati ya msitu wa adui. Tactically timu pinzani inakuwa bado haijatengeneza matundu ya kupitishia mpira. Kingine katika hizi mechi saba, Maximo kamgeuza Ngasa ndio kama kiungo mchezeshaji kule mbele. 

Mtazame Twite akipata mpira ni lazima aupeleke kwanza kwa Ngasa ambaye baadaye anajikuta ni lazima acheze kama play maker ili 8&9 wapande juu zaidi wakati yeye huliacha goli na kukaa na mpira chini kulia. Atafunga lini? 

Natumaini ujio wa Emerson utairudisha YANGA kwenye zama zake na Ngasa ataanza kufunga tena. Nane apewe Uhuru mkubwa wa kuchezesha timu ili washambuliaji wapokee pasi za mwisho nzuri.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!